
Wizara ya
afya ya Afghanistan imesema takriban watu themanini wameuawa na zaidi
ya wengine 150 wamejeruhiwa katika shambulio la kujitoa mhanga
lililofanyika kwenye mji mkuu Kabul.
Baadhi ya taarifa zinasema kulikuwa na milipuko miwili.
Shambulio
hilo linaonyesha kuwa lililenga maandamano ya maelfu ya watu kutoka
jamii ndogo ya Hazara, ambao hujikuta wakidhalilishwa na kufanyiwa
ukatili.
Walikuwa wakiandamana kupinga mpango wa serikali wa kuhamisha umeme kutoka kwenye majimbo yao katikati ya nchi.BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment