KAMPUNI
ya Chemi & Cotex inayotengeneza bidhaa za za afya ya Mdomo ya
Whitedent imezindua mchezo wa bahati nasibu wa kujishindia moja ya
magari 25 aina ya Suzuki Alto K10 jijini Dar es Salaam leo.
Bahati nasibu hiyo imezunduliwa na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk. Adelhelm Meru wakati wa kusherehe
madhimisho ya miaka 25 ya Whitedent jijini Dar es Salaam leo. Amesema
kuwa Kiwanda cha Chemi & Cotex kimeadhimishi miaka yake 25
kuwaajili ya kutekeleza kikamilifu agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli la Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.
Nae
Afisa Mwendeshaji Mkuu wa kampuni ya Chemi & Cotex, Raja
Swaminathan amesema kuwa katika kusherekea miaka 25 ya bidhaa ya
Whitedent wametaka kuwashirikisha wananchi wote katika mafanikio ya
kampuni yao.
Amesema
kuwa wananchi watawashirikisha kwa kuchezesha baahati nasibu hiyo ili
kujipatia zawadi ya gari ambayo ni Mpya kwa kuotea ndani ya gari kuna
maboksi mangapi kwa kujaza fomu ya kushiriki katika shindano hilo.
Mafanikio
makubwa ya Whitedent yanaonyesha kuwa uwezo wa Viwanda hapa nchini ni
mkubwa tunauwezo wa kukua na kutengeneza bidhaa bora kwa watanzania kwa
bei nafuu na pia kuuza ulimwenguni kote. amesema Swaminathan
Shindano
hili lililozinduliwa leo jijini Dar es Salaam pia limezinduliwa katika
mikoa ya Arusha, Dodoma, Mbeya, Mwanza na Musoma pia wanategemea
kuzindua katika mikoa ya Tabora, Kilimanjaro,Morogoro na Kigoma katika
kusherekea miaka 25 ya Whitedent hapa nchini.
Katibu
Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk. Adelhelm Meru
akizungumza wakati wa kusherekea miaka 25 ya Whitedent ilifanyika jijini
Dar es Salaam leo ikiwa sambamba na uzinduzi wa shindano la kukisia
idadi ya Pakiti za Whitedent zilizomo ndani ya gari moja ambapo shindano hilo litakuwa katika mikoa yote ya Tanzania.
Afisa Mwendeshaji Mkuu wa kampuni ya Chemi & Cotex, Raja Swaminathan akizungumza wakati wa sherehe za kusherekea kutimiza miaka 25 ya kampuni ya Whitent iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni Chemi & Cotex, M Balasubramanium akizungumza
wakati wa kusherekea miaka 25 ya Whitedent ilifanyika jijini Dar es
Salaam leo ikiwa sambamba na uzinduzi wa shindano la kukisia idadi ya
Pakiti za Whitedent zilizomo ndani ya gari moja ambapo shindano hilo litakuwa katika mikoa yote ya Tanzania.
Afisa Mwendeshaji Mkuu wa kampuni ya Chemi & Cotex, Raja Swaminathan wakifurahia jambo na Katibu
Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk. Adelhelm Meru wakati
wa kusherekea miaka 25 ya whitedent jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi
ya wafanyakazi wa kiwanda cha Chemi& Cotex wakiwa katika sherehe ya
kusherekea miaka 25 ya Whitedent iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Katibu
Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk. Adelhelm Meru
akiweka maboksi ya Whitedent katika gari jijini Dar es Salaam leo
kwaajili ya washiriki wa shindano hilo kubashiri katika mchezo wa bahati
nasibu kujua kama kuna boksi ngapi katika kila gari ambalo limewekwa
maboksi hayo.
m
Kikundi cha ngoma wakitumbuiza wakati
wa kusherekea miaka 25 ya Whitedent ilifanyika jijini Dar es Salaam leo
ikiwa sambamba na uzinduzi wa shindano la kukisia idadi ya Pakiti za Whitedent zilizomo ndani ya gari moja ambapo shindano hilo litakuwa katika mikoa yote ya Tanzania.
Baadhi ya wanakikundi wakiigiza igizo wakati wa kusherekea miaka 25 ya Whitedent jijini Dar es Salaam leo.
SHARE
No comments:
Post a Comment