TRA

TRA

Thursday, August 11, 2016

Afisa wa pili,timu ya Kenya arejeshwa nyumbani kwa udanganyifu

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Kocha wa Kenya,John Anzrah arejeshwa nyumbani
Kocha wa Kenya,John Anzrah arejeshwa nyumbani
Kocha wa timu ya riadha ya Kenya inayoshiriki michuano ya Olimpiki mjini Rio de Janeiro amerudishwa nyumbani kwa kosa la udanganyifu.
Mkuu wa Timu ya Olimpiki ya kenya, Kip Keino amesema John Anzrah aliigiza kama miongoni wa wakimbiaji wa mita 800, na kutoa sampuli ya mkojo kwa niaba ya mkimbiaji Ferguson Rotich.
Udanganyifu uligundulika na wakaguzi wa dawa za kusisimua misuli baada ya kuangalia picha za kitambulisho alichokuwa amevaa, ndipo walipogundua kuwa sura ya Bwana Anzrah haeindani na mchezaji aliyefanya uchunguzi.
Mkuu wa Timu ya Olimpiki ya kenya,Kip Keino amesema uongozi wa timu yake hautavumilia tabia hiyo ingawa mpaka sasa hakuna hatua yoyote iliyotolewa dhidi ya Rotich.
Anzrah ni afsa wa pili kutoka kenya kurejeshwa nyumbani, Wa kwanza akirudishwa kwa kosa la kuomba rushwa ili kuweza kukwepa upimaji wa matumizi ya dawa za kusisimua misuli.
Kumekuwa na idadi kadhaa ya wanariadha wa Kenya ambao walishindwa kufuzu vipimo vya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu huku ni wiki iliyopita tu shirika la kupambana na matumizi ya dawa hizo WADA likiiondoa Kenya kwenye nchi zilizoshindwa kutimiza masharti.BBC

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger