Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa ufafanuzi juu ya utozwaji wa kodi za
misaada inayotolewa na wadhamini kusaidia Sekta ya Maendeleo ya Michezo
Nchini.
Ufafanuzi
huo umetolewa jana na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi,
Richard Kayombo kutokana na habari iliyochapishwa kwenye baadhi ya
vyombo vya habari kuhusu Serikali kukosa mabilioni ya fedha kwa sababu
ya kutokukusanya kodi ya fedha zinazotolewa na wadhamini kwenda kwa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
“Fedha
zinazotolewa kama msaada kutoka kwa wadhamini huwa hazikatwi kodi lakini
TRA hupata mapato yake kutokana na matumizi ya fedha hizo hasa pale
wahusika wanapozitumia katika shughuli za kiuchumi”,alisema Kayombo.
Kayombo
ametaja baadhi ya shughuli za kiuchumi zinazoweza kuwaingizia mapato
kutoka kwenye misaada hiyo kuwa ni; kodi za waajiriwa wakiwemo makocha
na wachezaji, makusanyo ya uwanjani ,kupewa huduma za kitaalam pamoja na
majengo ya kupangisha au kupanga.
Amefafanua
kuwa kama Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) linakodisha jengo
basi fedha wanazopata lazima walipe kodi ya asilimia 10 kutoka kwenye
fedha hizo na kama wao ndio wamekodi jengo kwa ajili ya matumizi yao
wanatakiwa kutoa kodi ya asilimia 5.
Kwa
upande wa kodi kutoka kwa waajiriwa, Mamlaka hiyo inaendelea kutoa elimu
kwa vilabu vya michezo kuwa michezo ni ajira kama ajira zingine hivyo
mishahara yao inatakiwa kukatwa kodi kulingana na kiasi wanacholipwa.
Zoezi la kuwatoza kodi makocha na wachezaji limeanza rasmi mwaka huu.
Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment