Mkurugenzi
Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colasso akiongea wakati wa kutambulisha
kuhusu Money airtel kuingia ushirikiano na NMB banki ili banki ya NMB
ihudumie wakala wa Airtel Money.
Wakala wa Airtel kupata Airtel Money salio kwenye benki ya NMB popote.
Dar es
Salaam jumapili julai 31 kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia
huduma yake inayokuwa kwa kasi ya Airtel Money imeingia ubia na Benki ya
NMB ili kutoa huduma kwa wakala wake wanaotoa huduma za Airtel Money
kujipatia huduma ya salio na pesa taslim katika matawi ya benki hiyo
popote nchini.
Akiongelea
ubia huo, Mkurugenzi wa Airtel Bw, Sunil Colaso alisema “tunachofanya
Airtel na benki ya NMB ni mundelezo wa mikakati tuliyojiwekea ya
kuhakikisha tunaleta maendeleo katika huduma za kifedha nchini ili
wateja wetu wapate huduma za uhakika na nafuu. Pia kuwepo kwa sera bora
za udhibiti na uwekezaji itachochea wawekezaji kuendelea kuboresha na
kuweka miundombinu bora zaidi ya huduma ili kugusa mahitaji ya wateja
wengi”
Tunajisikia
fahari kuona NMB banki anakuwa nguzo muhimu ya kutoa huduma za Airtel
Money kwa kuwafikishia wakala wetu salio kila walipo ili waweze
kuhudumia wateja wetu, hii inaonyesha dhairi huduma za kifedha kwa
mtandao zinazidi kupanuka kutokana na jitihada na ubunifu wa watoa
huduma kwa lengo la kuwahakikishia wateja usalama na unafuu katika
kufanya malipo, Nina uhakika Tanzania itaendelea kukua katika swala la
huduma za fedha endapo tu kutakuwa na mahusiano ya wadau kibiashara kama
haya ya Airtel Money na Banki ya NMB”
“NMB
itahudumia wakala wetu zaidi ya 45,000 ili kuweka na kutoa salio la
Airtel Money wakati wowote katika matawi yao 160 nchi nzima, haya ni
maendeleo makubwa sana hata kwa biashara yetu”. alieleza Colaso
NMB na
Airtel inaingia Ubia kipindi ambacho Airtel Money pia imezindua kampeni
yake kabambe ya Mr Money kwa lengo la kuwafikishia wateja wake taarifa
za uhakika na unafuu katika huduma za Airtel Money. Airtel Money
imefanikiwa pia kuleta huduma pekee za mikopo isiyokuwa na maharti
magumu ya TIMIZA ambapo inawawezesha wateja na mawakala wake zaidi ya
milioni 2 kujipatia mikopo kila wakati.
SHARE
No comments:
Post a Comment