Akikabidhi madawati hayo,meneja mkuu wa mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo amesema Kampuni yake imekabidhi kiasi hicho cha madawati kwa lengo la kuunga mkono jitihada za mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupunguza uhaba wa madawati katika shule za msingi na sekondari. “Mgodi wa Buzwagi unaunga mkono jitihada zinazofanywa na rais wa awamu ya tano,Dkt. John Pombe Magufuli katika kumaliza tatizo la wanafunzi kukaa chini,tumeamua kutekeleza kwa vitendo jitihada hizo” ,alieleza Mwaipopo.
Akipokea
madawati hayo Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Bi Zainab Telack ameupongeza
mgodi wa Buzwagi kwa mchango wao uliolenga kuunga mkono jitihada za
mheshimiwa rais Magufuli, katika kuhakikisha kuwa watoto wote wanakaa
kwenye madawati. “Nimefarijika sana kuona mnaunga mkono
serikali,tulikuwa na upungufu wa madawati lakini kwa msaada huu wa
madawati mmesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo”,alisema Telack.
Aidha
Mkuu huyo wa Mkoa wa Shinyanga amewataka wakurugenzi wa halmashauri
zote katika mkoa wa Shinyanga kuwachukulia hatua kali za kisheria wazazi
wote wanaowaachisha masomo wanafunzi. Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Halmashauri ya mji wa Kahama Abeli Shija akishukuru kwa niaba ya
halmashauri za mkoa wa Shinyanga, ameupongeza Mgodi wa Buzwagi kwa
jitihada zao mbalimbali katika kutekeleza miradi ya kimaendeleo katika
mkoa wa Shinyanga na hususani wilaya ya Kahama.
Hafla
hiyo ya kukabidhi madawati ilifanyika Julai 28,2016 katika Shule ya
Msingi Majengo iliyoko wilayani Kahama katika halmashauri ya mji wa
Kahama ambapo ilihudhuriwa pia na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama
mkoa wa Shinyanga,viongozi wa wilaya ya Kahama,uongozi wa Mgodi wa
Buzwagi, walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Majengo.
Meneja
mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo(mwenye kofia ya bluu) akimpokea
mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack wakati wa hafla ya kukabidhi
madawati 4494 yaliyotolewa na Mgodi wa Buzwagi unaomilikiwa na Kampuni
ya uchimbaji wa madini ya ACACIA.
Wanafunzi wa shule ya msingi Majengo iliyopo katika halmashauri ya mji
wa Kahama wakipiga makofi kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakati
wa hafla ya kupokea madawati kutoka kwa uongozi wa Mgodi wa Buzwagi.
Wanafunzi
wa shule ya msingi Majengo moja ya shule zilizonufaika na mchango wa
madawati yaliyotolewa na Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi.

SHARE

No comments:
Post a Comment