Benki ya DCB COMMERCIAL imetoa madawati 100 kwa shule ya msingi Lubakaya iliyopo Kata ya Zingiziwa jijini Dar es Salaam, ikiwa ni ukamilishaji wa ahadi yake ya kuchangia madawati 300 kwa shule za manispaa tatu za mkoa wa Dar es Salaam.
Mkuu wa kukabiliana na majanga wa Benki ya DCB, Kulwa Deteba
akizungumza na waanafunzi pamoja na viongozi mbalimbali jijini Dar es
Salaam leo amesema kuwa benki ya DCB imeguswa na tatizo la ukosefu wa
madawati kwa shule ya msingi hapa nchini.
Amesema kuwa bodi na uongozi wa benki ya DCB inaunga mkono juhudi za
serikali katika kukabiliana na tatizo la madawati hapa nchini inetoa
madawati 100 katika shule ya Msingi Lubakaya jijini Dar es Salaam leo.
Nae Mkuu wa shule ya Msingi Lubakaya iliyopo kata ya
Zingiziwa, Said Chitumba amewashukueu benki ya DCB kwa mchango wao kwa
kutoa madawati 100 katika shule hiyo ikiwa shule hiyo inavyumba 16 vya
madarasa na sasa wanaukosefu wa madawati 300.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akikabidhiwa
madawati na Mkuu wa kukabiliana na majanga wa Benki ya DCB, Kulwa Deteba
jijini Dar es Salaam leo, madawati ambayo yatapelekwa katika shule Mpya
ya Lubakaya iliyopo Kata ya Zingiziwa jijini Dar es Salaam.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akikabidhiwa madawati na Mkuu
wa kukabiliana na majanga wa Benki ya DCB, Kulwa Deteba wakimkabidhi
madawati Mkuu wa Shule ya Msingi, Lubakaya (Katikati) jijini Dar es
Salaam leo. Katika Hafla iliyofanyika katika Shule ya Msingi Mnazi Mmoja
jijini Dar es Salaam leo.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko na Mkuu wa kukabiliana na
majanga wa Benki ya DCB, Kulwa Deteba wakiwa wamekaa kwenye madawati
mara baada ya kukabidhi madawati kwenye shule ya Msingi Lubakaya iliyopo
kata ya Zingiziwa jijini Dar es Salaam leo.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko madawati na Mkuu wa
kukabiliana na majanga wa Benki ya DCB, Kulwa Deteba wakiwa wamekaa
kwenye madawati na wanafunzi wa shule ya Msingi Mnazi Mmoja
wakiwawakilishi wanafunzi wa shule ya Msingi Lubakaya iliyopo kata ya Zingiziwa jijini Dar es Salaam leo.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko na Mkuu wa kukabiliana na
majanga wa Benki ya DCB, Kulwa Deteba wakiwa kwenye picha ya pamoja na
viongozi mbalimbali wa shule na wa serikali katika picha ya pamoja mara
baada ya kukabidhi madawati 100 kutoka benki ya DCB jijini Dar es Salaam
leo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Charles Kuyeko akizungumza katika Hafla Fupi ya Kuwakabidhi madawati 100 ya shule ya Msingi Lubakaya iliyopo kata ya Zingiziwa jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu
wa shule ya Msingi Lubakaya iliyopo kata ya Zingiziwa, Said Chitumba
akiwashukuru Benki ya DCB akiwashukuru benki ya DCB mara baada ya
kukabidhiwa madawati 100.
SHARE
No comments:
Post a Comment