Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mang’onyi wakati wa kutatua mgogoro kati ya wananchi na muwekezaji Shanta Gold Mine
Wanachi Kijijini Mang’onyi wakisikiliza kwa makini maelezo ya Mkuu wao wa Wilaya
Baadhi ya viongozi wakisikiliza maelezo ya awali katika ufunguzi wa mkutano huo uliodumukwa zaidi ya masaa matatu
Dc
Mtaturu akikemea tabia ya wanasiasa kutoa matamko ya kisiasa kwa maslahi
yao binafsi huku wakiwa mbali na eneo la wawakilishi wao.
Wananchi wakimlaki Mkuu wao wa Wilayaya Ikungi
Dc
Mtaturu akikemea tabia ya wananchi kuwachagua viongozi ambao wakipewa
ridhaa tu wanahamia Dar es salaam ilihali wananchi wao wanabaki kuteseka
pasina kuona umuhimu wa viongozi wao
Dc Mtaturu akitoa agizo kwa muwekezaji Shanta Gold Mine kuwalipa fidia haraka wananchi ili mradi huo uanze haraka iwezekanavyo
Nyumbani
ni salamu na unyumbani ni kuongea Kinyumbani, moja ya tabasamu kati ya
mwananchi na Dc wake wakizungumza kwa lugha moja baada ya mkutano
Wananchi
wakielemishwa na Mkuu wa wilaya juu ya siasa zinazokwamisha maendeleo
yao huku wanasiasa wenyewe wakishindwa kufanya uwakilishi katika maeneo
yao badala yake wamekuwa wawakilishi wa kitaifa
Msingi
wa kikao ni kusikilizana Mkuu wa Wilaya ya ikungi Miraji jumanne
Mtaturu, Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya, Uongozi wa Shanta Gold Mine
na wananchi Kijijini Mang’onyi wakiwa kwenye mkutano wa kutatua mgogoro
wao
Na Mathias Canal, Singida
Mgogoro
uliodumu katika kipindi cha zaidi ya miaka kumi kati ya wananchi wa
Kijiji cha Mang'oni na Muwekezaji Shanta Gold Mine umechukua sura mpya
ya maelewano baada ya wananchi kupatiwa elimu kuhusu umuhimu wa
uwekezekezaji na fursa watakazozipata ikiwa ni pamoja na ajira kwa
wananchi wenyewe na maendeleo ya Vijiji, Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa na
Taifa.
Akiwa katika kijiji cha Mang'onyi, Kata ya Mang'onyi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amezungumza
na wananchi hao kujua kadhia iliyopelekea kutoelewana kwa kipindi chote
hicho jambo ambalo limerudisha nyuma maendeleo tarajiwa kwa pande zote
mbili.
Mgogoro
huo umemalizika kwa Mkuu huyo kuamua kuwa wananchi walipwe fidia haraka
iwezekenavyo ili kupisha uanzishwaji wa Mgodi huo ambapo tayari
takribani wananchi 67 watalipwa katika awamu ya kwanza huku wengi zaidi
130 kulipwa katika awamu ya pili.
Dc Mtaturu amefanya
mkutano wake wa hadhara wa mwanzo tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi ambapo amewaagiza wawekezaji hao kukutana na kuwa na kikao cha
pamoja kati yao na wananchi waliofanyiwa tathmini kwa ajili ya
makubaliano ya namna bora ya malipo yao ikiwa ni pamoja na kuwashauri
kila mmoja kufungua Account Bank ili iwe rahisi na salama katika
uhifadhi wa fedha zao.
Baadhi
ya Wananchi katika kijiji hicho cha Mang'oni hivi karibuni walizuia
njia kwa kuweka magogo na mawe barabarani kama ishara ya kuwazuia
wawekezaji hao kupita katika eneo lao kwa madai ya kutolipwa fidia kwa
wakati na mwekezaji kuweka alama za mipaka ya eneo lake pasina wananchi
kushirikishwa.
Hata hivyo Dc Mtaturu alisema
kuwa huenda wananchi walikuwa na hoja ya msingi lakini kutolipwa fidia
hakumfanyi mtu kupata uhalali wa kuharibu mali za muwekezaji kwani
kufanya hivyo ni sehemu mojawapo inayochelewesha ulipaji wa fidia.
Mtaturu
ameonyesha kukerwa na viongozi wanaowapotosha wananchi hao ilihali
wakiwa wamejificha ama wanaishi mbali na kijijini hapo na kusema kuwa
hiyo ni nidhamu ya woga kwani muwakilishi mzuri wa wananchi ni yule
anayetanguliza maslahi ya wananchi mbele kuliko masalahi ya kisiasa,
Chama ama maslahi yake binafsi.
Mkuu
huyo wa Wilaya amesema kuwa kiongozi mzuri daima ni yule anayetatua
changamoto za wananchi sio kuzipinga kwani siasa safi na nzuri ni ile
inayoleta maendeleo sio kupinga maendeleo.
Amewataka
wawekezaji hao kuwa na mahusiano mazuri na wananchi kwani unapokuwa na
mradi wako katika Kijiji chochote nchini usipokuwa na mawasiliano mema
na wananchi wa eneo husika ni dhahiri kuwa mradi wako utakuwa hauna
tofauti na mradi mfu.
Hata
hivyo pamoja na faida kwa wananchi kulipwa fidia na serikali kupata pato
lake lakini wananchi 60 kutoka Kijijini hapo wataajiriwa katika Mradi
huo kati ya ajira 120 zilizopo ambapo wengine 60 watatoka nje ya eneo
hilo ili kutoa fursa kwa watanzania wote kujipatia ajira.
SHARE
No comments:
Post a Comment