Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis
Kigwangalla (kulia) akiwa nje ya Jengo la Kituo cha Tiba Asili na Tiba
Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED mara baada ya kufanya ziara ya
kushtukiza kufuatia mmiliki wa kituo hicho Tabibu Juma Mwaka kuendelea
kutoa matibabu kwa wagonjwa kwa siri pia kujitangaza kwenye vyombo vya
habari licha ya agizo la Serikali la Julai 11, 2016 la kumtaka asitishe
kutoa huduma zake kutokana na kukosa vigezo vya kisheria vya kumruhusu
kutoa tiba nchini.
Baadhi
ya Wagonjwa waliokutwa wakisubiri Tiba katika kituo cha Tiba Asili na
Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED kilichopigwa marufuku na Serikali
kutoa huduma zake nchini.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis
Kigwangalla (kulia) akizungumzwa na baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha
Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED waliokuwa wakitoa
huduma licha ya kituo hicho kupigwa marufuku na Serikali kutoa huduma
zake nchini.Kufuatia hali hiyo Naibu Waziri Dkt. Hamis Kigwangalla
ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata ndani ya saa 24 na kumfikisha
Mahakamani Mmiliki wa Kituo hicho tabibu Juma Mwaka kwa kukiuka agizo la
Serikali na kutoa huduma kinyume cha Sheria.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis
Kigwangalla (kulia), Mrakibu wa Polisi Ilala, E.M .Swebe (katikati) na
Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Dk. Paulo Mhame
(mwenye suti kushoto) kwa pamoja wakipitia kwa makini baadhi ya nyaraka
zilizokutwa ndani ya kituo cha Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN
(T) LIMITED kilichopo ilala Bungoni kufuatia upekuzi uliokuwa ukifanywa
na Jeshi la Polisi leo jijini Dar es salaam kwa lengo la kuchukua
vielelezo kama ushahidi wa Tabibu Mwaka kuendelea kutoa huduma kinyume
na sheria.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.
Hamis Kigwangalla (kulia), Mrakibu wa Polisi Ilala, E.M .Swebe
(katikati) na Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Dk.
Paulo Mhame (mwenye suti kushoto) na Mkaguzi wa Mamlaka ya Chakula na
Dawa nchini (TFDA) Dk. Itikija Mwanga wakiangalia baadhi ya dawa
zilizokutwa ndani ya kituo cha Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN
(T) LIMITED kilichopo ilala Bungoni kufuatia upekuzi uliokuwa ukifanywa
na Jeshi la Polisi leo jijini Dar es salaam kwa lengo la kuchukua
vielelezo kama ushahidi wa Tabibu Mwaka kuendelea kutoa huduma kinyume
na sheria.
Daftari
la lenye orodha ya mahudhurio ya wagonjwa lililokutwa dani ya kituo cha
Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED kilichopo ilala
Bungoni kufuatia upekuzi uliokuwa ukifanywa na Jeshi la Polisi leo
jijini Dar es salaam
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamis
Kigwangalla (kulia) akiongea na waandishi na wananchi waliojitokeza
kumsikiliza Naibu Waziri wa Afya Dkt. Hamis Kigwangala alipokuwa akitoa
msimamo wa Serikali wa kumchukulia hatua kali za kisheria Tabibu Juma
Mwaka wa kituo cha Tiba Asili na Tiba Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED
kwa kutoa huduma kinyume cha sheria.
Baadhi
ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza Naibu Waziri wa Afya Dkt. Hamis
Kigwangala alipokuwa akitoa msimamo wa Serikali wa kumchukulia hatua
kali za kisheria Tabibu Juma Mwaka wa kituo cha Tiba Asili na Tiba
Mbadala cha FOREPLAN (T) LIMITED kwa kutoa huduma kinyume cha sheria.
Picha/ARON MSIGWA -MAELEZO.
SHARE
No comments:
Post a Comment