Askari polisi akijaribu kuwatuliza waandamanaji waliokua wakiandamana dhidi ya serikali ya Ethiopia, Agosti 6, 2016.
Vikosi
vya usalama vya Wthiopia vinatuhumiwa kutumia nguvu zaidi na kusababisha
vifo vya watu zaidi ya 70 katika maandamano yaliyofanyika mwishoni mwa
juma lililopita katika majimbo ya Oromo na Amhara, makabila makuu mawili
nchini humo.
Shirika
la kimataifa la haki za binadamu Amnesty International limetoa ripotia
Jumatatu hii Agosti 8 ambapo limebaini kwamba watu 100 waliuawa katika
maandamano hayo na zaidi ya 110 walijeruhiwa.
Kiwango
cha matukio ya mwishoni mwa wiki ya Agosti 6 na 7 na na idadi ya vifo
vimeanza kuibua hali ya sintoifahamu nchini Ethiopia.
Mikusanyiko
na maandamano viilifanyika Jumamosi Agosti 6 katika jimbo linalokaliwa
na watu kutoka kabila la Oromo, ambalo ni kabila linaloongoza kwa watu
wengi nchini humo. Wakati huo ploisi ilitumia nguvu za kupita kiasi kwa
kuvunja maandamano hayo. Katika vijiji kadhaa, polisi iliwapiga
waandamanaji risasi za moto.
Maandamano
hayo,kwa mara ya kwanza, yalishuhudiwa katika mji mkuu wa nchi hiyo,
Addis Ababa, ambapo waandamanaji mia kadhaa walitawanywa kikatli.
Wahanga kadhaa katika jimbo la Amhara
Siku ya
pili, Jumapili, Agosti 7, maandamano yalisambaa hadi katika jimbo la
Amhara, kaskazini mwa nchi, pamoja na maelfu ya watu katika mji wa
kitalii wa Bahir Dar. Katika mji huo, kulishuhudiwa makabiliano kati ya
waandamanaji na polisi, ambayo yalisababisah vifo vya watu kadhaa.
Serikali
ya Ethiopia pia ilitaka kuzuia madhara ya wimbi hili la maandamano na
kukata kabisa mawasiliano ya simu na mitandao kwa karibu masaa 48 nchini
kote.
Oromo na Amhara, makabila mawili makubwa nchini Ethiopia yanaandamana kwa miezi kadhaa kwa sababu mbalimbali.RFI
SHARE
No comments:
Post a Comment