Askari
wa Kikosi cha Uokoaji cha Zimamoto wakizima moto uliokuwa ukiteketeza
ghala la Kampuni ya Boss Shopping Centre Ltd zilimo kuwa zikihifadhiwa
bidhaa mbalimbali eneo la Viwanda Chang'ombe jijini Dar es Salaam leo
mchana.
wananchi wakijadiliana jambo eneo la tukio.
Kazi ya uokoaji ikiendelea.
Askari wa uokoaji wakiwa kazini.
Mmoja wa wamiliki wa ghala hilo akisaini fomu ya uzimaji wa moto huo.
Moto ukiendelea kuwaka
Wananchi wakiwa eneo la tukio.
Na Dotto Mwaibale
MOTO
mkubwa umeteketeza ghala la Kampuni ya Boss Shopping Centre Ltd
lililokuwa likitumika kuhifadhia bidhaa mbalimbali maeneo ya viwandani
Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari eneo la tukio mmoja wa wamiliki wa ghala hilo
ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa kuwa hakuwa msemaji alisema moto
huo ulianza saa 9 mchana.
"Tumepata hasara kubwa katika ghala hili tulikuwa tukihifadhi friji, TV, sabufa kwa ujumla ni Boss Bland Home" alisema.
Alisema chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.
Baadhi
ya waokoaji walikuwepo eneo la tukio walilalamikia Kikosi cha Uokoaji
cha Zimamoto kwa kufika eneo la tukio bila ya kuwa na maji ya kutosha
hivyo kushindwa kuhudhibiti moto huo kwa wakati ambapo ilizuka taharuki
na kwa wamiliki wa viwanda vilivyokuwa jirani na ghala hilo.
Jitihada
za gazeti hili kumpata Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam, Simon Sirro ili kuzungumzia tukio hilo hazikuzaa matunda baada
ya kumpigia simu ambayo ilikuwa ikiita bila ya kupokelewa.
SHARE








No comments:
Post a Comment