Meneja
Ufadhili wa Miradi ya Elimu, Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Anne
Mlimuk (kushoto), akikabidhi akizungumza katika hafla yakupokea madawati
100 kutoka taasisi ya Jamani Foundation.
Mkurugenzi wa Jamani Foundation akizungumza katika hafla ya utoaji wa madawati 100 kwa Shule ya Msingi Yombo. Wanafunzi
wa Shule ya Msingi Yombo wakiwa wamekaa katika madawati waliyokabidhiwa
na taasisi ya Jamani Foundation. Kutoka kushoto, Mkurugenzi wa Jamani
Foundation, Nirmala Pabari, Meneja wa TEA, Tito Mganwa na Anne Mlimuka.Mkurugenzi
wa Jamani Foundation, Nirmala Pabari (kushoto) akikabidhi madawati
Mameneja wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Tito Mganwa (kulia), Anne
Mlimuka (wa pili kulia). Katikati ni Mwalimu Kasyupa kutoka Shule ya
Msingi Yombo akiwakilisha kwa niaba ya waalimu wa shule zilizopokea
msaada wa madawati 100.
Meneja Ufadhili wa Miradi ya Elimu, Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA),
Anne Mlimuk (kushoto), akikabidhi madawati yaliyotolewana JAMANI
Foundation kupitia TEA kwa mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Umoja, Juto
Komba.WanafunziwashuleyaMsingiyaMsingiUmojawakichezangomayaasili, kutumbuiza katika hafla ya makabithiano ya madawati.
Na Mwandishi Wetu
JAMII
imetakiwa kujenga utaratibu wa kutunza vifaa vya misaada vinavyotolewa
kwa ajili ya shule ili viweze kudumu na kusaidia wanafunzi kwa muda
mrefu.
Ushauri
Huo ulitolewa jana na Meneja wa Uhamasishaji na Wateja wa Mamlaka ya
Elimu Tanzania (TEA), Tito Mganwa wakati wakikabidhiwa madawati 100
yaliyotolewa na Jamani Foundation kwa shule za msingi Umoja na Yombo za
jijini Dar es Salaam.
Alisisitiza
umuhimu wa shule na wazazi kuwajengea watoto utaratibu wa kuthamini na
kutunza vifaa wanavyopewa ili viweze kuduma na kunufaisha wanafinzi
wengi zaidi kwa muda mrefu.
“Madawati
haya 100 yamegharimu 12m/-, hii inaonyesha ni jinsi gani wenzetu wa
Jamani Foundation wanathamini mahitaji yetu nasi basi kuonyesha shukrani
yetu tunapaswa kuyatunza ili yadumu na wenzetu wengine wafaidike pia na
msaada huu” alisema Mganwa.
Aliishukuru
Jamani Foundation kwa ushirikiano wao na Mamlaka ya Elimu katika
kuhakikisha kuwa wanaondoa kero zinazoikabili sekta ya elimu nchini ili
kuhakikisha ubora wa elimu unazingatiwa.
Amesema
kuwa taasisi hiyo imekuwa ikishirikiano nayo katika kukabiliana na kero
ya upungufu wa madawati na kwa sasa wanategemea kuanza ushirikiano
katika mradi wa ujenzi wa vyoo ili kutunza afya za wanafunzi mashuleni.
Akizungumza
wakati wa kuwakabidhi TEA madawati hayo, Meneja wa huduma za jamii wa
Jamani Foundation, Bi Nirmala Pabari alisisitiza umuhimu wa mashirika na
asasi mbalimbali kusaidia jamii ili kuboresha maisha.
Alisema
wataendelea kushirikiana na serikali katika maeneo mbali mbali
kulingana na mahitaji na uwezi wao lengo lao likiwa ni kuhakikisha kuwa
jamii inaishi katika mazingira bora ya upatikanaji wa huduma muhimu za
jamii.
Akipekea
madawati hayo, Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Umoja, Bw Dyuto Komba
alisema watatumia utaratibu wa kugawa kila dawati kwa mwanafunzi na
kuandikishana na wazazi wao ili kujenga dhana ya uwajibikaji.
“Kama
tulivyofanya kwenye kugawa kitabu, na kwa madawati hivyo hivyo, yatapewa
namba na majina ambapo kila mwanafunzi atapaswa kulitunza na
likiharibika mzazi au mlezi atawajibika kwa matengenezo” alisema.
Alisema
baada ya msaada huo, shule yake haina tena shida ya madawati na kusema
changamoto waliyonayo ni uhaba wa madarasa hasa kutokana na kuongezeka
kwa usajili wa wanafunzi wa shule ya awali na msingi.
SHARE
No comments:
Post a Comment