TRA

TRA

Thursday, August 4, 2016

KAIMU MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA ASIMAMISHWA KAZI KWA UZEMBE

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Captain Johnson Mfinanga na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Captain Sadick Muze kwa kosa la kuchagua rubani mmoja ambaye hajakidhi vigezo anavyotakiwa kuwa navyo marubani wanaotarajia kuondoka kesho kuelekea nchini Canada kwa ajili ya mafunzo ya kurusha ndege mpya mbili zinazotarajiwa kuwasili nchini katikati ya mwezi Septemba.
Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Kyela, Mkoani Mbeya Prof. Mbarawa amesema baada ya kukamilisha malipo ya awali ya ununuzi wa ndege mbili mpya kwa ajili ya ATCL alitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo kuwachagua marubani watano wenye vigezo ambavyo vinahitajika kwa ajili ya mafunzo hayo jambo ambalo amebaini mmojawapo wa waliochaguliwa hajatimiza vigezo na hivyo kuamua kumsimamisha kazi kwa kosa la uzembe.
Waziri Mbarawa amesisitiza kuwa msimamo wa serikali ni kuhakikisha kila mtumishi wa umma anatekeleza wajibu wake kwa kufuata sheria kanuni na taratibu hivyo atakaye kiuka msimamo huo Serikali haitasita kumchukulia hatua za kinidhamu.
Shirika la Ndege Tanzania katika mwaka huu wa fedha Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 500 kwa ajili ya ununuzi wa ndege tatu.(P.T)

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger