
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
(katikati) akiwa kwenye mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali za
Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) uliofunguliwa leo
kwenye ukumbi wa Mandvulo uliopo Lozitha, Swaziland.

Mfalme
Mswati wa III (kushoto) akihutubia kwenye ufunguzi wa mkutano wa 36 wa
Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC kwenye ukumbi wa Mandvulo, Lozitha
Swaziland.

Binti akionyesha bendera ya Tanzania wakati wa kuimba shairi maalum ya ufunguzi wa mkutano wa 36 wa SADC

Wakuu wa
nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika
(SADC) wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa mkutano
wa 36, Lozitha Swaziland.

Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisaini ubao wa kumbukumbu kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli wenye majina ya viongozi waliohudhuria
mkutano wa 36 wa SADC uliofanyika Lozitha, Mbabane Swaziland.
Mwenyekiti
anayemaliza muda wake wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika -SADC-
ambaye pia ni Rais wa Botswana Luteni Jenerali Dkt. Seretse Khama Ian
Khama amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo katika uchaguzi mkuu
uliofanyika mwaka jana.
Rais
huyo wa Botswana ametoa kauli hiyo ya pongezi katika hotuba yake kwenye
ufunguzi wa Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC
unaofanyika Mbabane- Swaziland ambapo Katika Mkutano huo Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dakta JOHN POMBE MAGUFULI anawakilishwa Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Rais huyo wa Botswana amesema ukuaji wa demokrasia katika nchi wanachama wa jumuiya ya SADC unaendelea
kuimarika hivyo ni muhimu jitihada hizo zikaendelezwa zaidi Amesema ana Imani kubwa na Viongozi waliochaguliwa kwa njia ya amani,uhuru na haki katika ukanda wa SADC akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Visiwa shelisheli kwamba watafanya kazi kwa bidii ili kuharakisha maendeleo kwa wananchi wao.
kuimarika hivyo ni muhimu jitihada hizo zikaendelezwa zaidi Amesema ana Imani kubwa na Viongozi waliochaguliwa kwa njia ya amani,uhuru na haki katika ukanda wa SADC akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Visiwa shelisheli kwamba watafanya kazi kwa bidii ili kuharakisha maendeleo kwa wananchi wao.
Wakuu wa
nchi na Serikali wa SADC katika mkutano huo wameshuhudia utoaji wa
zawadi mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika utunzi wa insha
na kwa wanahabari ambao wameandika habari mbalimbali kuhusu SADC
ikiwemo masuala ya huduma ya maji.
Aidha
Katika Mkutano huo wa 36 wa SADC viongozi wanaohudhuria watafanya
uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa SADC na Uchaguzi wa
Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Siasa, Ulinzi na
Usalama ( SADC Troika)
Katika
mkutano huo Wakuu wa nchi na serikali pia watapokea rasimu za maboresho
ya mikataba mbalimbali kutoka kwenye Baraza la Mawaziri kwa ajili ya
kutia saini. Miongoni mwa rasimu hizo ni mkataba wa kuboresha itifaki ya
SADC dhidi ya rushwa, maboresho ya itifaki ya ushirikiano wa siasa,
ulinzi na usalama ya SADC na maboresho ya itifaki ya biashara.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI (P.T)
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI (P.T)
SHARE








No comments:
Post a Comment