Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla amewaomba viongozi wa taasisi za Dini na viongozi wa dini
hapa Nchini kuhakikisha wanaendeleza maombi kwa kuliombea Taifa suala la
Amani ili Nchi kubaki katika misingi yake mikuu ya kuwaletea wananchi
wake Maendeleo pamoja na kudumisha amani iliyopo.
Naibu
Waziri Dk. Kigwangalla ameyasema hayo leo Agosti 14, 2016 wakati
alipokuwa mgeni rasmi kwa kumuakilisha Waziri wa Wizara hiyo. Mh. Ummy
Mwalimu katika kufunga kongamano la Kimataifa la siku nne la SHILOH
2016, lililoandaliwa na Kanisa la Victorious Church Of Tanzania (VCT)
lenye makao Makuu yake, Tabata Bima Jijini Dar es Salaam.
Katika
tukio hilo, Naibu Waziri aliweza kufunga rasmi kongamano hilo sambamba
na kutoa sadaka kwa akina Mama Wajane sadaka zilizoandaliwa na kanisa
hilo ilikuwasaidia akinamama Wajane mbalimbali.
Akitoa
neno la kupongeza kwa uongozi wa kanisa hilo, Naibu Waziri wa Afya Dk.
Kigwangalla ameeleza kuwa, hatua ya kanisa hilo kuwajali Wanamama Wajane
ni la kuungwa mkono kwani ni miongoni mwa mambo yanayopaswa kuigwa na
watu wote ambapo pia kwa hatua yao ya kuliombea amani Taifa pamoja na
viongozi wake ndilo jambo jema katika Nchi.
“Tunafanya
kazi hii ya uongozi ni kwa uwepo wake Mungu kwani uongozi wetu sie ni
Mungu ndiye aliyetaka tutumike na ndiye aliyetuita. Hivyo kufika kwangu
hapa ni kuitika wito wa kuwatumikia watu” alieleza Dk. Kigwangalla
wakati wa kutoa neno kwa waumini huku akinukuu moja ya vifungu vya
kwenye Biblia.
Ambapo
pia amewataka viongozi hao kuendelea kuzidisha maombi kwa kuimbea
Serikali ya Tanzania kwani kwa kipindi hiki ili Taifa liwe na amani
pamoja na wananchi wake wafanye mambo ya kimaendeleo.
Aidha,
katika hatua hiyo Dk. Kigwangalla alipata kuwafariji Wanawake Wajane
ikiwemo kukabidhi baadhi ya zawadi kwa akina mama hao mchango uliotoka
kanisani hapo.
Kwa
upande wake, Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo, Bishop Elis Musa Chessa
amemwelezea Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla kuwa ni miongoni mwa
Mawaziri wenye upeo mkubwa hivyo katika dhama za sasa ni kati ya
viongozi wanaohitajika katika kuinua Taifa kwani vigezo alivyo navyo
vinatosha kabisa kwa kipindi hiki na kuendelea kwa miaka ya baadae.
“Tunaiombea
Serikali yetu ya Tanzania kuwa na amani pamoja na viongozi wetu akiwemo
Rais Dk. John Pombe Magufuli. Viongozi wote wa Serikali pamoja na Jamii
nzima ya Tanzania” aliomba Bishop Elias Chessa.
Kongamano
hilo la Kimataifa la Shiloh 2016, lilianza Agosti 11 na kufikia tamati
siku ya leo Agosti 14 huku likikusanya waumini mbalimbali kutoka ndani
ya Tanzania na nje ya Tanzania.
Tazama MO tv, kuona tukio hilo hapa:
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla akipokelewa wakati wa kuwasilia kwenye kanisa hilo la
Victorious Church of Tanzania kufunga kongamano la siku nne la Kimataifa
la Shiloh 2016, mapema leo Agosti 14.2016
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea maua ya ukaribisho
Kiongozi
Mkuu wa Kanisa hilo la Victorous Church of Tanzania, Bishop Elis Musa
Chessa akimtambulisha Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla wakati akiwasili kanisani hapo
kwa viongozi wa dini na wageni waalikwa

Baadhi ya waumini wakipiga makofi kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa kuingia ukumbini
Baadhi ya waumini wakipiga makofi kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa kuingia ukumbini
Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo la Victorous Church of Tanzania, Bishop Elis Musa Chessa akitoa neno la shukrani katika tukio hilo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla katika kongamano hilo.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla akitoa neno la shukrani wakati wa kufunga rasmi kongamao
hilo la Shiloh 2016
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa neno la shukrani
Zoezi la kuwafariji Wamama Wajane likiendelea
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwafariji baadhi ya Wanamama Wajane
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwafariji baadhi ya Wanamama Wajane
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi Mkuu wa Kanisa
hilo la Victorous Church of Tanzania, Bishop Elis Musa Chessa nyuma ni
baadhi ya Akina mama Wajane waliofarijiwa wakati wa kongamano hilo

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa salamu kwa Akina mama hao
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla akiondola baada ya kumalizika kwa kongamano hilo
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla akizungumza machache kwa wanahabari (Hawapo pichani) wakati
wa kongamano hilo.
SHARE
No comments:
Post a Comment