
Mkuu
wa Kitengo cha Biashara za Serikalini NMB Bi. Domina Feruzi kulia
akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 206 Makamu Mwenyekiti wa
ALAT Bw. Stephen Mhapa kushoto kwa ajili ya mkutano wa 32 wa jumuiya
hiyo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es
salaam.

Makamu
Mwenyekiti wa ALAT Bw. Stephen Mhapa kushoto akiongea na waandishi wa
habari hawapo pichani kuhusu mkutano wa 32 wa ALAT utakaonza mwishoni
mwa Septemba mwaka huu , kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara za
Serikalini Bi. Domina Feruzi.Picha Na Ally Daud-Maelezo
Na Ally Daud-Maelezo
Rais wa
Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa 32 wa
Jumuiya ya Tawala za Mitaa Nchini (ALAT) ambao utafanyika mwishoni mwa
mwezi ujao mkoani Musoma.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Makamu Mwenyekiti wa
ALAT Bw. Stephen Mhapa amesema kuwa, katika mkutano huo wanatarajia Rais
Magufuli kuwa mgeni rasmi ili kufikia malengo ya mkutano huo.
“Tumeamua
kumuomba Mheshimiwa Rais kuwa mgeni rasmi kwa ajili ya kupata matunda
mema ya mkutano huo kutokana na kauli mbiu yake ya Hapa Kazi Tu ili
kuendana na kasi hiyo katika kuleta mendeleo na uongozi bora nchini,”
alisema Bw. Mhapa.
Aidha Bw.
Mhapa amesema kuwa uzinduzi wa mkutano huo utaendana na ukabidhishaji
wa zawadi kwa mshindi wa shindano la Halmashauri bora kwa mwaka 2016
ambapo mshindi atayechaguliwa na wananchi kwa wingi atakabidhiwa Trekta
yenye thamani ya shilingi milioni 56 ili kuinua shughuli za
kimaendeleo.
Mbali na
hayo Bw. Mhapa ameongeza kuwa mkutano huo utadhaminiwa na Benki ya NMB
kwa kupokea kiasi cha shilingi milioni 206 ambazo milioni 56 zitatumika
kugharamia zawadi na milioni 150 kugharamia mkutano huo.
Kwa
upande wa Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Serikalini kutoka benki ya NMB
Bi. Domina Feruzi amesema kuwa wameamua kufadhili mkutano huo ili
kurahisisha shughuli za kimaendeleo na kupata uongozi bora kwa faida ya
watanzania.
“Tumeamua
kudhamini mkutano huo ili kuweza kurahisisha shughuli za kimaendeleo na
kupata viongozi bora kwa kupitia mashindano ya Halmashauri Bora mwaka
2016,”amesema Bi. Domina.
ALAT
imekuwa na utaratibu wa kutoa zawadi kwa Halmashauri bora kwa mwaka wa
pili sasa ambapo imesaidia Halmashauri nyingi kufanya vizuri katika
ukusanyaji mapato na uboreshaji wa miundo mbinu na mazingira kwa ujumla.(P.T)
SHARE








No comments:
Post a Comment