Makamu wa
kwanza wa rais wa Sudan Kusini Thaban Deng Gai (Kushoto) akisalimiana
na rais Uhuru Kenyatta (Kulia) katika Ikulu ya rais jijini Nairobi
Agosti 16 2016
Makamu wa
kwanza wa rais wa Sudan Kusini Thaban Deng Gai ambaye amekuwa ziarani
nchini Kenya, amekanusha ripoti za kuwepo kwa mapigano ya mara kwa mara
jijini Juba au karibu na jiji hilo.
Gai
ambaye aliteuliwa na rais Salva Kiir mwezi uliopita kuchukua nafasi ya
Riek Machar, ameongeza kuwa mapigano ambayo yamekuwa yakiendelea katika
jimbo la Upper Nile na mji wa Wau yamesitishwa na kuna amani kwa sasa.
Hata
hivyo, amesema kama kuna mapigano yoyote, yanaendelea katika katika
jimbo la Equitorial Magharibi karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Congo, lakini kwa kiasi kikubwa nchi hiyo ina amani.
Makamu
huyo wa kwanza wa rais, alikutana na rais Uhuru Kenyatta siku ya
Jumanne, kujadiliana na kuhusu hatua iliyopigwa baada ya mazungumzo ya
viongozi wa Afrika Mashariki IGAD kuhusu hali ya usalama nchini humo.
Ujumbe wa Sudan Kusini na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi Agosti tarehe 16 2016
Ni ziara
iliyokuja baada ya Sudan Kusini kukubali azimio la Umoja wa Mataifa la
kutuma kikosi cha wanajeshi 4,000 kutoka Kenya, Ethiopia na Rwanda
kulinda amani na kuzuia mapigano jijini Juba, baada ya machafuko mpya
kuzuka mwezi uliopita.
Gai
ambaye alikuwa mshirika wa karibu wa Riek Machar, aliongoza ujumbe wa
waasi kufanikisha mazungumzo ya amani mwaka uliopita, amesisitiza kuwa
alikubali nafasi hiyo kwa sababu wanasiasa wa upinzani wanahitaji amani
ya kudumu.
Machar,
ambaye hajulikana alipo baada ya kuondoka Juba mwezi uliopita, amepinga
kuteuliwa kwa Gai na kusema yeye ndiye Makamu wa kwanza wa rais na rais
Kiiir hana mamlaka ya kumteua.RFI
SHARE
No comments:
Post a Comment