Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha
Bw. Mussa Juma akiongea na waandishi wa habari
Bw. Mussa Juma akiongea na waandishi wa habari
Na Woinde Shizza, Arusha
Chama
cha waandishi wa habari za michezo na Burudanimkoa wa Arusha (TASWA
ARUSHA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Arusha Media wameandaa tamasha
la 11 la waandishi wa habari za michezo na burudani kanda ya Kaskazini
ambalo litafanyika Septemba 11, 2016 katika uwanja wa Generat Tyre.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha, Mussa Juma
alisema zaidi ya watu 2500 wanatarajiwa kushiriki Tamasha hilo, ambapo
kutakuwa na michezo ya Soka, Kuvuta kamba, Mbio za magunia ,Kukimbiza
kuku na muziki kuanzia saa nne asubuhi hadi jioni.
Juma
alizitaja timu ambazo zitashiriki ni TASWA FC kutoka jijini Dar es
Salaam, timu ya Radio ORS kutoka mkoa wa Manyara, timu ya Sunrise
Radio, Timu ya chuo cha uandishi habari Arusha, timu ya MJ Radio na timu
ya Triple a Radio.
Katika
tamasha hilo, pia kutakuwa na timu za vyuo vya uandishi habari vya mkoa
wa Arusha, chuo cha habari Maalum, Tasisi ya habari na mawasiliano
iliyopo maji ya chai, TASWA Arusha.
“tamasha
litatanguliwa na semina ya siku moja ya wanahabari mkoani Arusha juu ya
masuala ya michezo, Utalii wa ndani na umuhimu wa Uwekezaji katika
taifa”alisema.
Mratibu
wa Tamasha hilo, Andrea Ngobole alifafanua kuwa pia kuna timu ambazo
zimealikwa ambazo ni Kitambi Noma, Timu ya TANAPA,timu ya TBL Arusha,
timu ya PEPSI na Coca Cola na Wenyeji timu ya Wazee Klabu.
Ngobole alisema Septemba 3, TASWA na Arusha Media watatangaza zawadi kwa washindi, wadhamini wote na Mgeni rasmi.
SHARE








No comments:
Post a Comment