TRA

TRA

Thursday, August 11, 2016

TBS YAKIFUNGIA KIWANDA CHA MIKATE

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !



Joseph Mabula

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limeanza kampeni ya kusaka na kufungia viwanda vya kuzalisha mikate visivyozingatia viwango vya ubora, pamoja na vinavyoendesha uzalishaji bila leseni ya ubora kutoka katika shirika hilo.

Msako huo ulianza jana Dar es Salaam ambako kiwanda cha kuzalisha mikate kiitwacho Heri cha Yombo Kigilagila katika Manispaa ya Temeke, kimefungwa kwa muda usiojulikana na wamiliki kuzuiwa kuendeleza uzalishaji, kwa sababu hizo pamoja na mazingira machafu ya uzalishaji.

Akizungumza muda mfupi baada ya kukifungia kiwanda hicho, Mdhibiti Ubora Mwandamizi kutoka TBS, Zainab Mziray, alisema shirika hilo litaendelea kufanya misako ya kustukiza ili kuhakikisha wazalishaji wa mikate na bidhaa nyingine nchini wanatekeleza matakwa ya viwango vya ubora katika uzalishaji.

Alisema kiwanda cha Heri kimekutwa kikizalisha mikate bila kufuata taratibu hasa katika eneo la viwango vya ubora, kwa sababu kimekuwa kikiendeshwa kiholela bila leseni ya shirika hilo, jambo linalothibitisha kuwa kilikuwa kikikiuka sheria ya viwango vya ubora.

“Wahusika wa kiwanda hiki wanazalisha kiholela na wanavunja sheria kwa sababu hawana cheti chochote cha ubora kinachoonesha kuwa wameruhusiwa kufanya uzalishaji huu wa mikate,” alisema Mziray.

Aliongeza kuwa, licha ya kukosa vyeti vinavyoonesha uhalali wa kuzalisha mikate hiyo kutoka TBS, hawana vyeti vya aina hiyo kutoka katika taasisi nyingine za serikali, jambo linalothibitisha kuwa wamekuwa wakifanya uzalishaji wa mikate hiyo ilimradi na kuhatarisha afya za walaji.

Kwa maelezo ya Mziray, mtu yeyote anaruhusiwa kuendesha biashara au kuzalisha bidhaa kama vile mikate ilimradi afuate sheria za nchi na taratibu za taasisi mbalimbali za serikali kama vile TBS kupewa nyaraka muhimu zitakazothibitisha kuruhusiwa kwao kutokana na kukidhi vigezo.

Kwa upande wake, mwakilishi wa mwenye kiwanda hicho aliyejitambulisha kuwa ni Byela George, alisema mmiliki alikuwa nje ya jiji hilo na kwamba aliwahi kumweleza kuwa anafuatilia masuala ya leseni ya ubora kutoka TBS.

Alikiri kuwa kwa kipindi hicho ambacho wakaguzi wa viwango wamefika kiwandani hapo, hawakuwa na cheti chochote kutoka taasisi yoyote ya serikali kinachoeleza jambo lolote kuhusu ubora wa bidhaa.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger