
Mwenyekiti
wa wafanyabiashara wadogowadogo katika eneo la mwenge lililopo katika
halimashauri ya Kinondoni,Bw Omary Hamis (kushoto) akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) akipinga
wafanya biashara wake wasi kubali kurubuniwa na wanasiasa katika mambo
ambayo hayana faida kwao (kulia) Sharifu Hasan.

Mwenyekiti
wa wafanyabiashara wadogowadogo katika eneo la mwenge lililopo katika
halimashauri ya Kinondoni,Bw Omary Hamis (katikati) akijibu maswali ya
waandishi wa habari wakati wa mkutano huo, kushoto ni Katibu wa Ulinzi
Shirikishi wa Wafanyabiashara wa eneo hilo, Dick Ponda, na kulia
Sharifu Hasan.
Na Mwandishi wetu-Dar es Salaam
MWENYEKITI
wa wafanyabiashara wadogowadogo katika eneo la mwenge lililopo katika
halimashauri ya Kinondoni, Omary Hamis amewataka wafanya biashara wake
wasi kubali kurubuniwa na wanasiasa katika mambo ambayo hayana faida
kwao.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam , alisema maranyingi vijana
ndio wamekuwa wakishawishiwa kuandamana hivyo wao meona hakuna umuhimu
wa kuandamana kwani kufanya hivyo hakuna faida kwao.
“Maranyingi
vijana wamekuwa wa kishwawishika na wana siasa kuandamana kitu ambacho
siyo chamsingi kwetu kama ambavyo tunashawishiwa tuandamane Septemba
mosi mwaka huu eti kisa kuna Oparesheni Ukuta, hivi kwani huo ukuta
unafaida gani kwetu, ifahamike kuwa hii nchi ni moja, Taifa letu n moja
sisi ni wamoja hivyo tusikubali kufanya maandamano yasiyo na tija
kwetu,” alisema Hamis.
Aliongeza
kuwa Rais John Magufuli ameonesha nia ya dhati ya kupambana na maadui
watatu amabao ni Maradhi, Ujinga na Umasikini hivyo hakuna sababu ya
kuacha kumungamkono kutoka na juhudi anazo zifanya za kujenga Taifa hasa
kwa kuwatetea wanyonge.
Naye
Katibu wa Ulinzi Shirikishi wa Wafanyabiashara wa eneo hilo, Dick Ponda
alisema Mfanyabiashara yoyote yule na vijana wote nchini atakama ni
mwanachama wa Chadema au chama chochote kile asikubali kushwawishika
kuandamana na Oparesheni ukuta kwani Rais wa nchi amekataza maandamano,
na kufanya hivyo kutasabisha madhara makubwa kwao.
Alisema
umefika wakati sasa vijana kujituma kwa bidii katika kufanya kazi, muda
uliopo ni wakufanya kazi na wala si siasa kama baadhi ya vyama wanavyo
fanya, Rais John Magufuli haangali chama katika utendaji wake hivyo kila
mtu anapaswa kuweka maswala ya chama chake pembeni.
Kwa
upande wake mmoja kati ya Wafanyabiashara hao, Fadhili Leuteni
alimpongeza mwenyekiti wao kutokana na ujasili wake wakuwakemea
wafanyabiashara wa eneo hilo.
“Mwenyekiti
wetu pamoja na viongozi wake wapo sahihi kwasabu maranyingi sisi ndio
tumekuwa tukitumiwa katika mambo ya uchochezi, hivyo na waomba wezangu
wasikubali kulubuniwa na wanasiasa kwani tutapata madhara makubwa ni
vyema kujiepusha,” alisema.(P.T)
SHARE








No comments:
Post a Comment