Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji (TIC), Clifford Tandari
akifafanua jambo wakati wa Kangamano la pili la Wahariri wa Habari
lililofanyika mapema leo kwenye Makao makuu ya Ofisi hizo jijini
Dar.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Bw.
Tandari alieleleza lengo kubwa la kukutana na Wahariri na wanahabari
kutoka vyombo mbalimbali ni kuwaeleza na kuwafanya watambue fursa na
mchango wa Kituo cha Uwekezaji wa kunadi miradi ya uwekezaji, Kuishauri
Serikali kuhusiana na masuala mazima yanayohusu uwekezaji na kuwahudumia
wawekezaji kwa mtindo wa “One Stop Centre”.
"Kama
sote tunavyofahamu uwekezaji nchini umechangia kwa kiasi kikubwa sana
kukuwa kwa uchumi wetu. Nchi ambayo haivutii wawekezaji na kutengeneza
mazingira mazuri ya biashara kamwe haiwezi kufanikiwa katika uchumi
wake. Kubwa zaidi ni kwamba Tanzania inashindana na nchi zingine zote
duniani katika kuvutia wawekezaji hao hao, hali ambayo inatuhitaji kuwa
makini zaidi na jinsi tunavyowahudumia wawekezaji wa ndani na wale wa
nje wanaotaka kuja kuwekeza nchini mwetu" alisema Bw. Tandari.
Bw.
Tandari alisema kuwa TIC kwa sasa imejipanga katika kuandaa mpango
mkakati ambao utaweza kurahisisha Utekelezaji wa majukumu ya Kituo na
kusimamia utekelezaji wa maagizo na malengo yake, Alisema kuwa wanaamini
mpango mkakati huo utarahisisha Usimamiaji wa shughuli na mipango yao
na kwamba wanategemea mpango mkakati huo utaweza kusaidia Kituo
kuhakikisha Utekelezaji wa Majukumu yao unaendana na mahitaji ya Mpango
Mkakati wa Miaka Mitano.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Uwekezaji (TIC).Clifford Tandari
akifafanua mambo mbalimbali kuhusiana na sula zima la uwekezaji hapa
nchini wakati wa Kangamano la pili la Wahariri wa Habari lililofanyika
mapema leo jijini Dar.
Bw.
Tandari alieleza kuwa Kituo cha Uwekezaji kina mkakati maalumu wa
kuhakikisha upatikanaji wa Sera na Sheria Mpya ya Uwekezaji kwani ile ya
awali imepitwa na wakati. "Sera yetu ya Uwekezaji pamoja na Sheria
vimepitwa na wakati na haviendani na mazingira ya sasa na tupo kwenye
taratibu za kufanyia marekebisho sera na sheria ili kuhakikisha
vinakidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye ya nchi yetu katika masuala
yanayohusu Uwekezaji"alisema Bw. Tandari.
Alisema
kuwa Vivutio vingi wanavyopewa wawekezaji vinalenga kuwapa nafasi ya
kuanza kuzalisha bidhaa zao mapema na hivyo kuwa na uwezo wa kulipa kodi
katika muda mfupi zaidi. "Kwa misingi hii kivutio kikubwa kuliko vyote
ni huduma wanayoipata kutoka serikalini kuwa bora, ya haraka na isiyo na
ukiritimba unaozaa usumbufu mkubwa kwa wawekezaji.
"Mkakati
wa Serikali ni kukiwezesha Kituo chetu kuboresha huduma bora chini ya
“One Stop Shop” kwani ni muhimu sana katika kuondoa usumbufu kwa
wawekezaji na kujenga mazingira bora ya uwekezaji kwa wote. Mwekezaji
hana haja ya kuzunguka ili kupata vibali mbalimbali. Badala yake Anapata
huduma ya vibali hivi kupitia Kituo Cha Uwekezaji" alisema Bwa.Tandari .
Meneja Mahusiano wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) Pendo Gondwe akiratibu mijadala iliokuwa ikiendelea wakati wa Kangamano la pili la Wahariri wa Habari.lililofanyika mapema leo makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar.
Baadhi
ya Makaimu Wakurugenzi wa TIC wakifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa
kwenye wakati wa Kangamano la pili la Wahariri wa Habari.lililofanyika
mapema leo makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar.
SHARE
No comments:
Post a Comment