(Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog).
First
National Bank Tanzania imetangaza washindi wa droo ya pili ya kampeni
yake ya kuhamasisha uwekaji akiba. Kupitia droo iliyofanyika makao makuu
ya benki hiyo jijini Dar es salaam leo jumla ya washindi kumi
wamejishindia shilingi milioni moja kila mmoja kupitia mpango huo wa
kuwahamasisha Watanzania kuwa na utamaduni wa kujiwekea akiba benki.
Akiongea
jijini Dar es salaam leo, Mkuu wa Kitengo cha wateja wa rejareja wa FNB
Tanzania, Francois Botha alisema mbali na kuhamasisha uwekaji akiba,
kampeni hiyo inalenga kuhimiza wananchi wote nchini ambao hawajafungua
akaunti benki kujitokeza na kuweka akiba. Kupitia droo hiyo ya pili,
shilingi milioni kumi imetolewa kwa jumla ya washindi kumi ambao ni
Gabriel Mrosso wa Mwanza, Agnes Mndasha wa Dar es salaam, Ebenezer Moshi
wa Mwanza, Amiri Mziray wa Dar es salaam, Nelis Kashanga wa Mwanza,
Festo Msofe wa Dar es salaam, Daniel Kakesyo wa Mwanza, Boniface Likingo
wa Dar es salaam, Michael Lusana wa Mwanza, Benedicto Makoye wa Dar es
salaam.
Botha
aliwapongeza washindi hao na kuongeza kwamba benki hiyo inaendelea
kufanya jitihada kubwa kuboresha huduma na kuongeza kwamba kampeni hii
ni sehemu ya jitihada hizo zilizolenga pia kuongeza idadi ya watumiaji
huduma za kibenki nchini. Kupitia kampeni hiyo inayofanyika kwa muda wa
miezi mitatu, wateja wa FNB waliopo na wateja wapya wanaingizwa kwenye
droo moja kwa moja kutokana na kila shilingi elfu hamsini wanayoweka
akiba katika benki hiyo.
Jumla
ya washindi 30 watanufaika kupitia kampeni katika muda wa miezi mitatu.
Click here to Reply or Forward 2.02 GB (13%) of 15 GB used Manage Terms
- Privacy Last account activity: 21 minutes ago Details Cathbert
Kajuna's profile photo Cathbert Kajuna Show details
SHARE
No comments:
Post a Comment