Jumla ya watu 51 waliuawa katika usiku wa Jumamosi 13 kuamkia Jumapili Agosti 14 nje ya jiji la Beni.
Nchini
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, katika mkoa wa Kivu Kaskazini, watu
wanaendelea kukimbia eneo lililo karibu na mji wa Beni. Usiku wa
Jumamosi 13 kuamkia Jumapili, Agosti 14, kwa mujibu wa asasi za kiraia,
watu 51 waliuawa, wengi kwa visu. mauaji haya yalihusishwa waasi wa
Uganda wa ADF.
Baada ya
kiongozi namba mbili wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO)
Jumatatu wiki hii, ujumbe wa serikali umewasili Jumanne hii asubuhi
katika mji wa Beni. Ujumbe huo ukiongozwa na Waziri Mkuu umezuru eneo la
Rwangoma, katika kichaka, ambapo kulitiokea moja ya mauaji.
Kulikuwa
na Waziri Mkuu wa DRC Augustin Matata Ponyo, Naibu Waziri Mkuu wa Mambo
ya Ndani na Usalama, Evariste Boshab. Baraza lote la Ulinzi limzuru
maeneo mbalimbali ya mauaji ya mwishoni mwa wiki iliyopita. Ziara
iliyofanywa kwa usafiri wa gari, lakini pia viongozi hao walitembea kwa
mguu katika kichaka katika eneo la Rwangoma, Mbelu ambapo piakulitokea
mauaji. Ujumbe huu ulikua umezungukwa na idadi kubwa ya vikosi vya
usalama na kuongozwa na Mkuu wa mji wa Beni.
Mkuu wa
mji wa Beni alieleza kuwa hapa watu watano waliuawa - walikuwa
walifungwa kamba, huku nyumba moja ikichomwa moto- baadhi ya watu
waliuawa na wengine walijeruhiwa au walinusurika. Ujumbe ulikuwa na
mtazamo wa kile kilichotokea, na hilo ndio lengo la ziara iliyoagizwa na
rais wa Jamhuri, hivyo ndivyo alivyosema Waziri Mkuu Augustin Matata
Ponyo. Ziara ya kufanya tathmini ya hali iliyotokea na kujaribu kuelewa
kile kilichotokea katika nje kidogo ya mji wa Beni.
Hatua za kipekee zaahidiwa
Pia kulikuwa na majadiliano mengi kuhusu kama kulikuwa na ulaji njama. majibu meengi pia yaliyotolewa na Mkuu wa mji wa Beni: .
Ujumbe wa
Waziri Mkuu wa Congo, Augustin Matata Ponyo, J"Hapana ilikuwa njia ya
kawaida inayotumiwa na wasi waADF-Nalu kati ya ngome yao ya Mwalika na
'eneo hili la mauaji' "Jumanne hii asubuhi katika mji wa Beni ulikuwa
kwanza kusema kuwa kitendo hiki kiliyotokea ni cha kigaidi.
Waziri
Mkuu pia amesisitiza kuwa alitumwa, yeye pamoja na Baraza la Ulinzi, na
rais wa jamhuri, ambaye hakuweza kuzuru mji wa Beni, na kwamba
watajaribu kujadili uwezekano wa kukabiliana na hali hii ya kipekee kwa
sheria za kipekee, ambazo zitachukuliwa hivi karibuni, baada tu ya
tathmini hiyo kuwasilishwa kwa Rais Joseph Kabila. RFI
SHARE
No comments:
Post a Comment