Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
WIZARA
ya Fedha yaombwa kuongeza Bajeti ya huduma za uzazi za Dharura hadi
kufikia asilimia 100 ili kuokoa maisha ya kinamama na watoto wa changa
wakati wa kujifungua.
Ameyasema
hayo Mratibu wa Kitaifa wa White Ribbon Alliance, Rose Mlay wakati
akitoa mafuzo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, amesema
kuwa Serikali iweke wigo wa fedha zinazopangwa kwaajili ya kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi isitumike kwa shughuli nyingine.
Rose
amesema kuwa Vifo vitokanavyo na uzazi havivumiliki, wilaya zote za
kila mkoa ziweke kipengere cha huduma kamili za uzazi za zarura(CEmoNC)
ili kuondokana na vifo vya mama na mtoto wakati wakujifungua.
Amesema
kuwa vifo vingi vya akina mama na watoto vinatokana na mambo mbalimbali
hasa ukosefu wa huduma kamili za Uzazi za Zarura katika hospitali,
upungufu wa Damu salama na kuwa na wakunga wasio na ujuzi katika
hospitali.
Mratibu
wa Kitaifa wa White Ribbon Alliance, Rose Mlay akizungumza na waandishi
wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kutoa mafunzo juu ya
kutokomeza Vifo akinamama na watoto wachanga vitokanavyo na uzazi.

Mtoa Maada na Mshauri wa Maswala ya Habari, Chiku Lweno akitoa maada kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Meneja
Mtetezi wa Mradi wa The White Ribbon Allince, Sizarina Hamisi akitoa
ufafanuzi wa jambo wakati wa kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi
ya waandishi wa habari waliohudhulia katika mafunzo hayo yaliyotolewa
na wafanyakazi wa White Eibbon Allince jijini Dar es Salaam leo.
SHARE












No comments:
Post a Comment