Uamuzi
wa Serikali wa kuzuia daladala zinazofanya safari kati ya Mbezi Louis
na Mkoa wa Pwani kutofika Kituo cha Simu 2000 kilichopo Ubungo jijini
Dar es Saalam umekuwa mwiba kwa wananchi wa maeneo hayo kutokana na
kupaa kwa gharama za usafiri.
Baadhi
ya wananchi waliohojiwa na gazeti hili wamesema tangu Serikali
ilipozuia magari kufika katika kituo hicho wanalazimika kuongeza bajeti
ya nauli kwa siku kwa wastani wa Sh500 tofauti na ilivyokuwa awali.
Awali,
baadhi ya wananchi hao walikuwa wanatumia magari mawili kutoka
Chalinze, Mlandizi, Ruvu na Kibaha kuingia jijini hapa, lakini sasa
wanalazimika kutumia magari matatu mpaka manne kufanikisha safari zao.
SHARE
No comments:
Post a Comment