
Upinzani
nchini Venezuela umeahidi kuendelea kumshinikiza rais wa nchi hiyo,
Nicolas Maduro, baada ya maelfu ya waandamanaji kumiminika njiani katika
mji mkuu wa Caracas.
Waandamanaji
hao wanataka kuitishwe kura ya maoni ya kumuondoa madarakani kiongozi
huyo, kabla ya Januari 10. Iwapo Maduro atashindwa katika kura hiyo ya
maoni, italazimika kufanyike uchaguzi wa mapema.
Kiongozi
wa upinzani wa chama cha Democratic Unity Roundtable, Jesus Torrealba,
ameliambia shirika la habari la AFP kwamba yalikuwa ni maandamano
makubwa kuwahi kutokea katika miongo kadhaa iliyopita. Alisema kuwa kati
ya watu 950,000 hadi milioni moja na laki moja walijitokeza katika
maandamano hayo. Na wameahidi kuendelea na shinikizo hilo hadi pale rais
wa nchi, Nicolas Maduro,
"Leo
ndiyo mwanzo wa jitihada zetu tukiwa pamoja na raia wote wa Venezuela,
wanaotimiza haki yao ya kikatiba ya kuandamana kwa amani hadi pale
kutakapopatikana mabadiliko ya kikatiba na yaliyo ya kidemokrasia,”
amesema Jesus Torrealba.
Waandamanaji
waliokuwa wamevalia nguo vyeupe walikuwa wakipiga mayowe wakisema
"Venezuela imekumbwa na njaa. Na serikali hii lazima itaanguka."
Wananchi wa Venezuela wanalalamikia hali mbaya ya uchumi, pamoja na uhaba wa chakula na madawa.
Hali
ilibadilika na kuwa ya wasiwasi wakati maandamano hayo yakiendelea.
Serikali ya Maduro iliwakamata wanaharakati kadhaa pamoja na kutuma
vikosi vya polisi katika kila kona ya mji na kuonya kutatokea umwagikaji
wa damu.
Wafuasi wa Maduro pia walijitokeza
Kundi
dogo la watu waliokuwa wamejifunika nyuso huku wakirusha mawe,
walikabiliana na polisi karibu na mwisho wa maandamano hayo. Polisi
ilitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya na pia iliwatia mbaroni
baadhi ya vijana miongoni mwao.
Sambamba
na maandamano hayo ya upinzani, wafuasi wa rais Maduro nao waliandamana
kumhakikishia kiongozi huyo kwamba wapo naye pamoja, wengi wao wakiwa ni
watumishi wa serikali. Idadi ya wafuasi wa Maduro waliojitokeza
inakadiriwa kuwa watu 30,000.
Akiwahutubia
wafuasi wake, Maduro aliwaambia kuwa upinzani unapanga mapinduzi dhidi
yake kama yale yaliyoiondoa kwa muda mfupi serikali ya mtangulizi wake,
Hugo Chavez mwaka 2002.
"Tumewakamata
wanachama kadhaa wa ngazi za juu wa siasa za mrengo wa kulia ambao
walitaka kufanya mapinduzi. Walikuwa na mipango ya kutega mabomu,
walimiliki silaha, pamoja na maelfu ya dola ya fedha haramu. Walikuwa na
mipango ya kuwashambulia watu wao wenyewe," amesema Nicolas Maduro.
Baada ya
kauli yake hiyo, upinzani umetangaza mipango ya kufanya maandamano
mengine mawili ya kitaifa, ya Septemba 7 yatazilenga ofisi za tume ya
uchaguzi na ya pili yatafanyika Septemba 14.
Matumaini
ya upande wa upinzani ni kushinikiza kuitishwa kwa kura ya maoni ya
kumuondoa Maduro madarakani kabla ya mwaka huu. Iwapo Maduro atashidwa,
kutaitishwa uchaguzi mkuu wa mapema na upinzani unatarajiwa kushinda
kulingana na utafiti wa maoni ya jamii. Lakini kama kura hiyo
itacheleweshwa hadi baada ya Januari 10 na Maduro akashidwa, makamu wake
wa rais atalazimika kumpokea wadhifa wa urais hadi muhula wake utakapo
malizika mwaka 2019.DW
SHARE








No comments:
Post a Comment