Mkuu wa
Kitengo cha Uhusiano na uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti
wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Sarah Kibonde Msika (katikati)
na Bw. Kenneth Batanyita (kushoto), wakitoa maelezo kuhusu Hifadhi ya
Jamii kwa mgeni aliyetembelea banda la SSRA, wakati wa maonesho ya Wiki
ya Fedha, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkuu wa
Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Bi. Sarah Kibonde Msika
akitoa maelezo na kugawa vijarida kuhusu hifadhi ya Jamii kwa baadhi ya
wageni waliotembelea banda la SSRA katika maonesho ya Wiki ya Fedha,
viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Afisa wa
SSRA, Bi. Amina Ally akitoa mada katika Semina ya uhamasishaji wa
Hifadhi ya Jamii kwa wajasiriamali wadogo walioshiriki katika mafunzo
yaliyokuwa yakitolewa katika Wiki ya Fedha yaliyofanyika viwanja vya
Mnazi Mmoja hivi karibuni.
Maofisa
wa Mamlaka, Bi. Imani Masebu (kushoto) na Bi. Agnes Lubuva (kulia)
wakitoa maelezo kuhusu umuhimu wa Hifadhi ya Jamii kwa wajasiriamali
wadogo waliotembelea banda la SSRA katika maonesho ya wiki ya Fedha hivi
karibuni.
Afisa wa
Mamlaka Bw. Athumani Juma akigawa vipeperushi na vijarida vya
uhamasishaji wa umuhimu wa kujiunga na Hifadhi ya Jamii kwa
wajasiriamali wadogo waliotembelea banda la SSRA katika maonesho hayo,
hivi karibuni.
Afisa wa
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),
Bw. Ally Masaninga akitoa maelezo kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na
Mamlaka pamoja na kugawa vipeperushi kwa washiriki waliotembelea Banda
la SSRA katika maonesho ya wiki ya Fedha, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini
Dar es Salaam.
Afisa wa
SSRA, Bw. Frank Kilimba akitoa maelekezo kuhusu Sekta ya Hifadhi ya
Jamii kwa wageni waliotembelea banda la Mamlaka hiyo, katika viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini.
Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista
Mhagama (wa pili kushoto), katika meza kuu akiwa na viongozi wa maonesho
ya wiki ya Fedha pamoja na wawakilishi wa Mashirika na Taasisi
mbalimbali ikiwemo SSRA, wakifuatilia kwa makini risala toka kwa
wajasiriamali (hawapo pichani), katika siku ya kilele cha maonesho ya
Fedha, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam hivi karibuni. (P.T)
SHARE








No comments:
Post a Comment