Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumsalimia
aliposimama Nangurukuru, wilaya ya Kilwa mkoani Lindi wakati akiwa
njiani kuelekea mkoa wa Mtwara ambapo atakuwa na ziara ya kikazi ya siku nne.
Sehemu ya Wakazi wa Nangurukuru mkoani Lindi wakishangilia ujio wa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumsalimia alipowasili kwenye
ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambapo atakuwa na ziara ya kikazi ya
siku nne.
Makamu wa
Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi katika mji wa
Nangurukuru Wilaya ya Kilwa waliojitokeza kwa wingi wakati akipita
kuelekea Mkoani Mtwara kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu.
Makamu wa
Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi alipokuwa
akiwasalimia wananchi katika mji wa Nangurukuru Wilaya ya Kilwa
waliojitokeza kwa wingi wakati akipita kuelekea Mkoani Mtwara
Baadhi ya
wananchi aliojitokeza kumlaki Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu
wakati akipita kwenye mji wa Nangurukuru wilayani Kilwa mkoa wa Pwani.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema
serikali itatuma kikosi maalum cha kukabiliana na uvuvi haramu
unaoendelea katika bahariili kudhibiti na tatizo hilo ambalo limeathiri
sana mazalia ya samaki na kuchangia kupungua kwa samaki baharini.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 7-Sept-2016 wakati
akisalimiana na wananchi wa Nangurukuru wilayani Kilwa mkoani Lindi
ambao walijitokeza kumsalimia wakati akielekea mkoani Mtwara katika
ziara yake ya kikazi ya siku NNE mkoani huo.
Makamu wa
Rais amesema katika kuhakikisha kazi hiyo inafanyika vizuri serikali
pia itatuma wataalamu wa mazingira ambao watafanya tathmini ya uharibifu
wa mazingira katika bahari ili kujua uharibifu uliofanyika na kuchukua
hatua ya kukabiliana na hali hiyo.
Ameeleza
kuwa serikali itachukua hatua hizo ili kuinusuru bahari kwa sababu
imekuwa ni chanzo kizuri ya mapato kwa wananchi kutokana na shughuli za
uvuvi na shughuli nyingine zikiwemo za utalii.
“Bahari
yetu ndio mapato yetu, bahari yetu ndio maisha yetu tumeitumia vibaya
mapato yamepungua na maisha hayawi mazuri hivyo ni muhimu tuitunze ili
iendelee kutulea kwa manufaa mazuri.”
Kuhusu
uboreshaji wa huduma za afya kwa wananchi wa Kilwa, Makamu wa Rais Samia
Suluhu Hassan amesema serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti
zinazolenga kuhakikisha wananchi wote nchini wanapata huduma bora za
afya katika ngazi zote.
Amesema
mpango huo wa uboreshaji wa huduma za afya kwa wananchi nchini utaenda
pamoja na utoaji wa elimu bora wa wanafunzi kote nchini chini ya mkakati
wa serikali wa kutoa elimu bure kuanzia wanafunzi darasa la kwanza
hadi kidato cha nne.
Katika
ziara yake mkoani Mtwara, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Samia Suluhu Hassan kesho 8-Sep-16 atazindua jengo la ofisi za
Tume ya Maadili ya Uongozi wa Umma Kanda ya Kusini na kukagua miradi
mbalimbali ya maendeleo mkoani humo.
SHARE
No comments:
Post a Comment