
Na Georgina Misama-MAELEZO
Mpaka
kufikia 2021 serikali imeahidi kusambaza umeme wa kutosha na wa uhakika
katika vijiji vyote nchini ili kuendana na dhamira ya kuelekea katika
uchumi wa kati kupitia viwanda.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo wakati
wa kipindi cha TUNATEKELEZA kinachorushwa na Televisheni ya Taifa ya
TBC1 kwa ushirikiano na Idara ya Habari-MAELEZO.
Prof.
Muhongo alisema kuwa kukamilika kwa miradi ya kuzalisha nishati ya umeme
ikiwemo Mradi wa Kinyerezi 1 unaozalisha megawati 150 kwa siku
umesaidia kuongeza upatikanaji wa huduma ya umeme wa kutosha mijini na
baadhi ya vijiji.
“serikali
sasa ipo katika kutekeleza miradi mikubwa ya nishati za umeme na gesi
ikiwa ni jitihada za kuhakikisha mpaka kufikia 2021 vijiji vyote nchini
viwe vimepata huduma ya nishati ya umeme”. Alisema Prof. Muhongo
Aidha,
Prof. Muhongo alisema kuwa utekelezaji wa Miradi hiyo unaenda sambamba
na lengo la Serikali ya awamu ya Tano ya kuwa na uchumi wa kati kupitia
viwanda ifikapo 2025.
Akizungumzia
kuhusu mikakati ya kuthibiti utoroshaji wa madini nchini Prof. Muhongo
alisema kuwa serikali inaendelea kuweka mikakati ya kuwakamata
watoroshaji wa madini hasa katika maeneo ya mipakani na viwanja vya
ndege.
Prof.
Muhungo alisema kuwa kuanzia mwaka 2012 wamekamata madini ya aina
mbalimbali zaidi ya Tani 10 yaliyokuwa yanatoroshwa kutoka nchini kwenda
nchi mbalimbali.
Prof.
Muhongo amewataka watanzania kutumia fursa mbalimbali zitakazotokana na
utekelezaji wa miradi katika sekta ya gesi na mafuta ili kujiongezea
kipato na kuiwezesha nchi kutimiza malengo yake kuelekea kuwa nchi ya
uchumi wa kati.(P.T)
SHARE








No comments:
Post a Comment