
Na.Alex Mathias.
Baada ya
kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Toto African ya jijini Mwanza,Kocha
Mkuu wa klabu ya Yanga Hans Van Der Pluijm ameitangazia vita Kagera
Sugar zitakapokutana kesho kwenye uwanja wa Kaitaba mechi ya Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania bara.
Akizungumza
baada ya kutua mkoani Kagera Pluijm,amesema kuwa anategemea mchezo
utakuwa mgumu kwa kila timu kutafuta alama tatu muhimu na ukiangalia
wenyeji nao wana alama 18 sawa na sisi ila hilo halitupi shida.
“Kila
mechi kwetu tunaichukilia kwa uzito wa aina yake na ukiangalia kikosi
changu bado kina uchovu wa mashindano ya kimataifa ndio maana najaribu
kufanya mabadiliko mbalimbali ili kuwapa nafasi wachezaji wote
wacheze”alisema Pluijm
Timu hizo
zinatarjia kukutana kesho huku zikiwa zote zimetoka kupata ushindi
Kagera waliwafunga Maafande wa JKT Ruvu kwenye uwanja wa Mabatini wakati
Mabingwa watetezi wao waliwafunga wadogo zao Toto mabao 2-0.
Hata
hivyo Kocha huyu hakuacha kumsifia mshambuliaji wake raia wa Zambia
Obrey Chirwa kwa kuanza kuzoea Ligi na kuanza kujiamini na kufunga
magoli mpaka sasa anayo mawili na kuondoa presha za mashabiki ambao
walikuwa wanaomuona kama sio mchezaji mzuri.
Kagera
Siugar wanawakaribisha mabingwa wao wakiwa chini ya Kocha mpya Mecky
Mexime na wakiwa nafasi ya nne kwa alama 18 wakati Yanga wapo nafasi ya
tatu kwa alama 18 huku kinara bado Simba anaongoza kwa alama 24. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment