TRA

TRA

Sunday, November 6, 2016

AFRICAN LYON YAISAMBARATISHA SIMBA UWANJA WA UHURU MCHEZO WA LIGI KUU TANZANIA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


lyom-1024x683
Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
Timu ya African Lyon imeharibu sherehe za Simba katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam baada ya kuwatandika goli 1-0 mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania bara na kuvunja mwiko wa wekundu wa Msimbazi kucheza bila kufungwa.
Kwa matokeo hayo yameifanya Lyon kufunga pazia la mzunguko wa kwanza kwa ushindi mnono na Simba walikuwa wamecheza mechi 13 bila kupoteza hata mchezo mmoja msimu huu.
Aliyepeleka kilio Msimbazi ni kinda la zamani la Yanga B,Abdallah Msuhi dakika za majeruhi 90 baada ya uzembe wa beki pamoja na kipa wa Simba kujichanganya na kumkuta mfungaji katika nafasi nzuri na kuipandisha Lyon nafasi ya tisa wakiwa na pointi zao 17.
Licha ya kufungwa Simba inabaki kileleni mwa msimamo wa Ligi wakiwa na pointi 35 na mchezo wao wa mwisho wa kufunga mzunguko wa kwanza wanaenda kumaliza mkoani Mbeya dhidi timu ya Tanzania Prisons mchezo utakaopigwa uwanja wa Sokoine siku ya Jumatano.
Simba wanatarajia kusafiri LEO kuelekea mjini Mbeya kucheza na Prisons ambao nao wamejeruhiwa kwa kufungwa na mabingwa watetezi Yanga goli moja kwa bila lililofungwa na Simon Msuva na kufanya tofauti ya pointi 5 ya Ligi hiyo.(P.T)

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger