Meneja wa
Uendeshaji wa kampuni ya Multichoice Tanzania akiongea na waandishi
hawapo pichani wakati wa uzinduzi huo uliofanyika kwenye hoteli ya
Serena jijini Dar es salaam..
Msanii Lucas Mhavile “Joti” akiongea na waandishi pamoja na maofisa kutoka kampuni ya DStv wakati wa uzinduzi huo.
Katikati
ni Balozi wa DStv Bomba Lucas Mhavile “Joti” akiwa na Ofisa Masoko wa
DSTV Alpha Mria kulia na kushoto ni Meneja Uendeshaji Multchoice Bw.
Baraka Shulukindo.
Na.Alex Mathias,Dar es salaam.
Msanii wa
Vichekesho, Lucas Mhavile (Joti) ,ametangazwa rasmi kuwa balozi wa
Kampuni ya Multichoice Tanzania (DStv) kupitia kifurushi cha DStv Bomba
ili kuweza kupeperusha bendera ya kifurushi hicho pamoja na kukitangaza
katika jamii ya Watanzania.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Dar es Salaam jana, Meneja Uendeshaji wa Kampuni
hiyo, Ronald Shulukindo amesema kuwa wameamua kumchagua msanii huyo
kwasababu wanajua anakubalika katika jamii na wanategemea ataweza
kuwatangaza vyema tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo watanzania wachache
wamekuwa na uelewa wa bidhaa zao.
“Tunatambua
ya kwamba joti ni msanii mkubwa hapa nchini na tumeamua kumchagua kuwa
balozi wa kifurushi chetu cha Bomba ili aweze kwenda kutilia mkazo kwa
wateja wetu ambao hawajui huduma bora zinazotolewa na kampuni hii na
kupitia yeye tunahakika watanzania watakuwa na uelewa mkubwa wa hizi
huduma zinazopatikana hapa kwetu,” alisema Shelukindo.
Aidha
Shelukindo amesema kuwa kuelekea kwenye msimu wa siku kuu ya Chrismas
pamoja Mwaka Mpya wamefanya maboresho ya kifurushi cha Bomba kwenye
upande wa gharama pamoja na idadi ya channeli ili kuweza kutoa fursa kwa
idadi kubwa ya watanzania waliokuwa wameshindwa kumudu gharama kubwa
zilizokuwa zikihitajika wakati wa kutoa huduma.
Amesema
kuwa kampuni hiyo imekuwa na tabia ya kusikiliza maoni yanayotolewa na
wateja wao ili kuweza kuboresha huduma zao na kutokana na hali ngumu ya
kimaisha iliyopo hivi sasa imewapelekea kufanya mabadiliko yatakayotoa
nafasi kwa kila mteja au mtanzania kumudu gharama hizo.
Kwa
upande wa msanii Joti amesema kuwa kwanza anamshukuru Mungu kwa
kuteuliwa katika nafasi hiyo na pia atashirikiana na DStv kuweza
kufikisha ujumbe kwa wateja na kuwa moja ya Kifurushi safi cha Bomba
kwani kitakuwa na mambo mengi ya kujifunza.
“Mimi
huwa sifanye kazi kwa kuwaagusha watu nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu
kuweza kufikisha ujumbe katika jamii na ukizingatia hakuna raha kama
DStv hivyo watanzania wote tumeamua kuwapunguzia gharama ili kuendana na
kasi ya maisha kwa watu wote na DStv ipo kwa ajili ya watu na huwa
inajali kila Mteja”alisema Joti
Hata
hivyo wametaja kauli mbiu ya msimu huu ni “Ni Zamu Yetu”-Ni zamu yako
wewe mteja kupata kilicho bora zaidi na ni zamu yetu sisi Multichoice
kukuhudumia kwa kukupa kilicho bora zaidu kwa bei nafuu.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment