Na.Alex Mathias.
Baada ya
kufungwa magoli matatu na Brazil hatimaye Leo timu ya Argentina
wameibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Colombia mchezo uliochezwa
kwenye uwanja wa Estadio De Bicentenario wa kuwania nafasi ya kufuzu
kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Argentina
walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa nahodha na mchezaji wa
kutengemea wa klabu ya Barcelona Lionel Messi dakika ya 10 akifunga goli
safi akitumia udhaifu wa mabeki wa Colombia na kuwanyanyua mashabiki wa
Argentina waliofurika katika uwanja huo.
Lucas
Pratto aliifungia tena Argentina magoli mawili ya haraka haraka katika
dakika za 23 na 28 na kuwafanya Colombia wapotee kwa kuchanganikiwa na
hayo magoli matatu hadi timu zinaenda mapumziko wenyeji walikuwa mbele
kwa magoli matatu kwa bila.
Kipindi
cha pili kilikuwa kigumu kwa kila timu kwani zilishindwa kufungana na
Colombia wakishindwa hata kupata goli la kufutia machozi hadi mwamuzi
toka nchini Eduardor ,Zambrano anamaliza mpira Argentina wameibuka na
ushindi wa magoli 3-0 na kuwapandisha juu ya msimamo.
Sasa
Argentina imepanda hadi nafasi ya tano wakiwa na pointi 19 huku Colombia
nao wakishuka chini nafasi ya sita wakiwa na pointi 18 na matokeo
mengine,Eduador 3-0 Venezuela,Chile 3-1 Uruaguay,Peru 0-2 Brazil.
VIKOSI:
Argentina: Romero;
Mercado, Otamendi, Funes Mori, Mas; Mascherano, Biglia; Di Maria (Acuna
85′), Banega (Perez 63′), Messi; Pratto (Higuain 79′)
Subs: Roncaglia, Rulli, Guzman, Pizarro, Demichelis, Correa, Zabaleta, Belluschi, Aguero.
Goals: Messi, Pratto.
Booked: Funes Mori, Mercado, Banega, Pratto
Colombia: Ospina;
Arias, Sanchez, Murillo, Balanta; Sanchez, Cuadrado, Torres (Copete
67′), Barrios (Torres 46′), Rodriguez; Falcao (Bacca 76′)
Subs: Cardona, Perez, Gonzalez, Muriel, Vargas, Medina, Borja, Diaz, Aguillar.
Booked: Alvarez, Arias, Rodriguez, Cuadrado (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment