Jamhuri
ya Kidemokrasi ya Congo imeimarisha doria zake mipakani baada ya
kiongozi wa kijeshi wa zamani wa kundi la waasi la M23 kutoweka kwenye
kambi iliowakusanya wapiganaji wa zamani katika nchi jirani ya Uganda.
Julien
Paluku gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini nchini Congo amesema maafisa wa
serikali wa Uganda hawajuwi mahala alipo Sultani Makenga ambaye alikuwa
kiongozi wa kijeshi wa kundi la waasi la M23 katika Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo.
Paluku
ameliambia shirika la habari la Uingereza Reuters hapo Jumamosi kwamba
wamekuwa na mawasiliano na idara ya ujasusi ya Uganda ambao
wamethibitisha kwamba kanali huyo wa zamani huenda ametoroka tokea
Ijumaa na majasusi wa Uganda wanashindwa kujuwa mahala alipo.
Afisa wa
kitengo cha kisiasa wa kundi la M23 amekataa kuzumgumzia juu ya kadhia
hiyo kwa kusema kwamba masuala kuhusu Makenga waulizwe maafisa wa
Uganda. Msemaji wa jeshi la Uganda amesema hajuwi iwapo Makenga
ametoweka lakini atafuatilia kujuwa mahala alipo.
Milio ya risasi yahanikiza Bunagama
Afisa wa
forodha wa Congo katika mji wa Bunagama amesema milio ya risasi
ilisikika wakati wa usiku katika milima inayouzunguka mji huo ambacho ni
kituo muhimu cha kuvuka mpaka kuingia Uganda na ilikuwa ngome ya kundi
la M23.Milio ya risasi iliendelea kusikika hadi Jumamosi asubuhi.
Afisa
huyo amesema hawajuwi milio hiyo ya risasi ilikuwa ikitokea wapi na
hawajui nini kinachotokea kutokana na kwamba jeshi haliwaambii kitu
chochote.Afisa huyo aliyekataa kutajwa jina kutokana na kutoruhusiwa
kuzungumza na vyombo vya habari amesema harakati za kijeshi zimeongezeka
katika mji huo wa Bunagana halikadhalika uwepo wa kijeshi wa wanajeshi
wa Uganda upande wa pili wa mpaka katika mji wa Kisoro.
Paluku
amesema hakuna uthibitisho kwamba Makenga amerudi Congo lakini
kumekuwepo na repoti ya kuwepo kwa vikosi visivyojulikana katika Mbuga
ya taifa ya Sarambwe inayopakana na mpaka.Gavana huyo amesema "Kuna hali
kubwa ya tahadhari.Vikosi vyetu viko katika doria ya mapambano ili
kwamba jambo hilo ikiwa ni la kweli waweze kumdhibiti Makenga na
washirika wake anaoandamana nao."
Hadi
kushindwa kwake hapo mwaka 2013 kundi la M23 lilikuwa na nguvu kubwa
kabisa miongoni mwa makundi kadhaa ya wapiganaji ambayo yalikuwa
yakiendelea kudhibiti maeneo makubwa yenye utajiri wa madini ya
mashariki mwa Congo licha ya kumalizika kwa vita vya mwaka 1998-2003.
Uvumi kuungana upya wapiganaji wa M23
Eneo hilo
linaendelea kuwa hatari kutokana na mgawanyiko wa kikabila na
kisiasa.Wakati ilipofikia kilele cha umashuhuri wake kundi hilo la M23
liliuteka mji mkuu wa Kivu ya Kaskazini wa Goma lakini kufuatia
kushindwa kwake na majeshi ya Umoja wa Mataifa na yale ya Congo
wapiganaji wake wengi walikimbilia Uganda na Rwanda. Tokea wakati huo
wamekuwa wakiishi katika makambi yanayosimamiwa na wanajeshi wakisubiri
misamaha walioahidiwa chini ya makubaliano ya amani.
Hao mwaka
2014 Uganda ilisema ilikuwa ikiwahifadhi wapiganaji wa zamani wa kundi
hilo 1,430. Hata hivyo wengi wao tayari wameondoka kwenye makambi hayo
na uvumi umekuwa ukizidi kuhanikiza kwamba waasi hao wanajiandaa
kuungana tena.
Wachunguzi
wa Umoja wa Mataifa wamesema kundi hilo linalotuhumiwa kwa uhalifu wa
kivita na mashirika ya kutetea haki za binaadamu linaungwa mkono na
Rwanda madai ambayo serikali ya nchi hiyo imekuwa ikiyakanusha mara kwa
mara. DW
SHARE
No comments:
Post a Comment