Reince Priebus alionekana na Donald Trump usiku wa siku ya uchaguzi
Rais
mteule wa Marekani, Donald Trump, amemteua mwenyekiti wa kamati ya taifa
ya chama cha Republican, Reince Priebus, kutumika kama mkuu wa
wafanyakazi.
Bwana
Priebus ana uhusiano wa karibu na spika wa baraza la wawakilishi Paul
Ryan. Wandishi wa wa habari wanaarifu kwamba uteuzi wa Piebus unaweza
kuwaudhi wafuasi wake wa hali ya chini na hii inaashiria kwamba uongozi
ujao unalenga kufanya kazi kwa karibu na baraza la Congress
kujihakikishia ushindi wa mapema wa baraza hilo.
Stephen Bannon aliacha kazi yake ya awali na kuwa kampeni meneja wa Donald Trump
Stephen
Bannon, alikuwa ni mwenyekiti wa taasisi ya Breitbart News, ambayo ni
tovuti yenye maoni ya mrengo wa kulia , naye ameteuliwa kwa nafasi ya
mkuu wa mipango na mshauri mwandamizi.
Mkuu wa
wafanyakazi ambaye anafanya kazi kama mruhusu na mtengeneza ajenda kwa
rais, na kwamba ni mmoja wa chaguo muhimu la mapema kwa rais ajae.
Katika
taarifa yake, Trump alinukuliwa akiwazungumiza Priebus na Bannon ni
viongozi wenye sifa za hali ya juu waliofanya kazi pamoja wakati wa
kampeni zake za kuingia Ikulu ya Marekani.BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment