Mlezi wa
Kamati ya Miss Tanzania ambaye pia Balozi wa Heshima wa Botswana nchini
Tanzania, Bw. Emanuel Ole Naiko akimkabidhi bendera Diana Edward Lukumai
Miss Tanzania 2016 anayeondoka nchini kesho kuelekea nchini Marekani
kwa ajili ya Shindano la Miss Word linalotarajiwa kufanyika nchini humo,
Katikati ni Hashim Lundenga Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania,
Hafla hiyo imefanyika leo kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es
salaam.
Diana
Edward Lukumai Miss Tanzania 2016 akizungumza mbele ya waandishi wa
habari leo kwenye hoteli ya New Africa Jijini Dar es salaam wakati
alipokabidhiwa bendera ya Taifa kwa ajili ya safari yake ya Marekani
atakakoshiriki shindano la dunia la Miss Word, Kulia ni Mkuu wa Itifaki
Miss Tanzania Bw. Albert Makoye na katikati ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Miss Tanzania Bw. Hashim Lundenga.
Mapema
mwezi Machi 2016 tulishuhudia uzinduzi wa mashindano ya Miss Tanzania,
uzinduzi ambao ulifanyika katika Hotel ya Ramada iliyopo eneo la ufukwe
wa bahari ya Hindi Kunduchi.
Uzinduzi
wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2016 mwezi Machi kulianzisha
marathoni ya kumtafuta Miss Tanzania 2016 mashindano ambayo yalifanyika
katika mikoa mbalimbali nchini na hatimae kuweza kumpata mrembo wa
Taifa, Miss Tanzania 2016 Diana Edward Lukumai ambaye leo hii tunamuaga
aweze kutuwakilisha vema katika Mashindano ya urembo ya Dunia ambayo kwa
mwaka huu yatafanyika Washington DC nchini Marekani.
Katika
miaka 22 ya Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania, miaka yote hiyo
Fainali za shindano la Miss Tanzania lilikuwa likifanyika jijini Dar es
salaam, lakini kwa mwaka huu 2016 kwa mara ya kwanza Fainali hizi
zimefanyika jijini Mwanza, na napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru
wakazi wa Mwanza na vitongoji vyake kuweza kujitokeza kwa wingi katika
Fainali zile ambazo zilifanyika katika ukumbi wa Rocky City Jijini
Mwanza.
Mshindi
ameshapatikana ni mrembo wetu kutoka Kanda ya Kinondoni, Kituo cha
Ubungo. Miss Tanzania 2016 Diana Edward Lukumai na leo hii tupo hapa
kumfanyia sherehe maalumu ya kumuaga na kumtakia kila la heri katika
safari yake hii kuelekea Mashindano ya urembo ya Dunia tukiwa na
matumaini makubwa kwamba utatuwakilisha vema na kujerea na Taji la
Mrembo wa Dunia, yaani Miss World 2016.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment