Viongozi
wa Ulaya wako Berlin kutaka kuhakikishiwa na Rais Barack Obama wa
Marekani juu ya mkondo ambao yumkini ukafuatwa na rais mteule wa
Marekani Donald Trump kutokana na ahadi zake kuweza kutibua mfumo wa
dunia,
Rais
Obama amekaririwa akisema "Kujitolea kwetu kwa Ulaya ni kwa kudumu na
misingi yake iko katika maadili tunayoshirikiana maadili ambayo Angela
ameyataja,kujitolea kwetu kwa demokrasia,kujitolea kwetu kwa utawala wa
sheria,kujitolea kwa utu wa watu katika nchi zetu na katika dunia.
Muungano wetu wa washirika wetu wa NATO umekuwa msingi wa sera ya kigeni
ya Marekani kwa takriban miaka sabini katika nyakati mbaya na nzuri na
kwa kupitia marais wa vyama vyote viwili na kwa sababu Marekani ina
utashi wa msingi kwa utulivu na usalama wa Ulaya."
Rais
Barack Obama wa Marekani alitowa kauli hiyo katika mkutano wa pamoja na
waandishi wa habari mjini Berlin hapo Alhamisi (17.11.2016) ambao pia
ilihudhuriwa na mwenyeji wake Kansela Angela Merkel wa Ujerumani.
Fadhaa ya
kuchaguliwa kwa Trump imewatia wasi wasi viongozi wa Ulaya kutokana na
kiongozi huyo kuhoji mkataba wa usalama uliodumu kwa takriban miaka
sabini wa washirika wa Marekani chini ya kivuli cha Jumuiya ya Kujihami
ya NATO pamoja na kuahidi kujitowa katika mikataba iliopatikana kwa
tabu ya mabadiliko ya tabia ya nchi na kudhibiti mpango wa nyuklia wa
Iran.
Kujipendekeza kwa Putin
Kujipendekeza
kwake kwa Rais Vladimir Putin wa Russia pia kumezusha masuali juu ya
msimamo wake juu ya hatua ya Russia kumuunga mkono Rais Bashar al Assad
katika vita vya Syria na halikadhalika dhima ya Russia katika mzozo
mashariki mwa Ukraine.
Kabla ya
kufanyika kwa mazungumzo hayo Obama alikuwa na matumaini ya hadhari
kwamba Trump anaweza kubadili msimamo wake mara ataposhika wadhifa huo
wa urais.Amesema mtu inabidi awe makini akiwa katika wadhifa huo
venginevyo hutoweza kudumu kwa muda mrefu kwani matatizo yatakuja
kukuumbuwa.
Obama
amesema anatumai kwamba rais mteule atakuwa na mtizamo ule ule wa tija
kutafuta nyanja ambapo wanaweza kushirikiana na Russia pale maadili
yao, utashi wao vinakwenda sambamba lakini rais mteule atakuwa tayari
kusimamama dhidi ya Russia pale inapokiuka maadili yao na kanuni za
kimataifa.
Kubadilishana mawazo
Mkutano
wa leo kati ya Obama na viongozi wa Uingereza, Ufaransa,
Ujerumani,Italia na Uhispania ni wa kwanza kufanyika tokea kuchaguliwa
kwa Trump.
Mkutano
huo utatowa nafasi ya kubadilishana mawazo hadharani kwa njia isio rasmi
juu ya masuala muhimu ya kimataifa mathlan mada nzito ya mapambano
yanayongozwa na Marekani dhidi ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu
nchini Syria na Iraq halikadhalika suala la mzozo wa wahamiaji barani
Ulaya.
Obama
amesema Umoja wa Ulaya unaendelea kuwa mojawapo ya mafanikio makubwa ya
kisiasa na kiuchumi duniani mafanikio ambayo hayapaswi kuchukuliwa
kijujuu.DW
SHARE
No comments:
Post a Comment