Mwanamke mmoja
nchini Brazil ambaye alikuwa akijihusisha na uwekaji wa vifaa vya kukuza
maumbile ya kike kinyume cha sheria amekufa katika shambulio lenye
viashiria vya ulipizaji kisasi baada ya upasuaji ambao haukuzaa matunda.
Wakati akikaribia kifo chake, alikabiliwa na mkono wa sheria mahakamani kwa kosa la kujifanya daktari.
Polisi mjini Rio de Jeneiro wanamsaka mwanamume aliyeonekana kwenye mkanda wa video wakati akiingia nyumbani kwa mwanamke huyo usiku wa jumamosi, kabla ya mwili wa mwanamke huyo kuonekana mtaa wa jirani.
Wachunguzi wanaoufanyia utafiti mwili huo wanaeleza kuwa mwili wa bi Gama, ulishuhudiwa huku mikono ya mwanamke huyo ikiwa imefungwa kwa nyuma, na kwamba uso wake ulionesha kuwa ulishambuliwa.
Ndugu wa bi Gama wameshangazwa na taarifa za kuwa ndugu yao alijiita daktari kwani wao wanadai kutokuwa na taarifa hizo, na mara zote wakati wa uhai wake alikuwa akiwaonya wateja wake juu ya matokeo ya upasuaji wa kuongezewa silika.
SHARE
No comments:
Post a Comment