Waziri wa Ulinzi wa Japan amesema kuwa makombora yaliyorushwa na
Korea Kaskazini yameanguka katika eneo la bahari la Japan, takriban km
300 kutoka ufukwe wa Kaskazini Mashariki wa nchi hiyo. Awali, maafisa wa
Japan na wa Korea Kusini walithibitisha kuwa Korea Kaskazini imerusha
makombora manne yaliyopigwa marufuku, kama jibu kwa mazoezi makubwa ya
pamoja ya kijeshi kati ya Marekani na Korea Kusini, ambayo serikali ya
Korea ya Kaskazini inayachukulia kuwa maandalizi ya uvamizi dhidi yake.
Bado hakuna uhakika kuhusu aina ya makombora yaliyorushwa na Korea
Kaskazini, lakini mnamo miezi ya hivi karibuni nchi hiyo imefanya
mfululizo wa majaribio ya makombora ya masafa mbalimbali. Waziri Mkuu wa
Japan Shinzo Abe amesema jaribio la leo linadhihirisha kuwa Korea
Kaskazini imekuwa kitisho kipya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment