Mbunge
wa jimbo la Kigoma Mjini, Zitto Zuberi Kabwe amefungukia juu ya Mauaji
yanayoendelea mkoani Pwani na kudai maeneo matatu ya Mkuranga, Kibiti na
Rufiji hatajawahi kupatiwa majibu ikiwa ni mtu wa 31 akiwa ameuawa
usiku wa kuamkia leo.Zitto
amefunguka hayo baada ya Taarifa za kifo cha Mwenyekiti wa CCM Tawi la
Njia Nne katika Kijiji cha Muyuyu Wilayani Kibiti, Iddy Kirungi,
kuthibitishwa kwa mwenyekiti huyo ameuawa kwa kupigwa risasi na watu
wasiojulikana.
"Eneo
la #MKIRU ( Mkuranga, Kibiti, Rufiji) halijapata jawabu la kudumu, Huyu
mtu wa 31 kuuawa eneo Hilo"Akithibitisha kutokea kwa mauaji hayo Kaimu
Mkuu wa Wilaya ya Kibiti, Juma Njwayo,ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya
Rufiji na kusema kwamba, marehemu alipigwa risasi akiwa nyumbani kwake
wakati akijaribu kukimbia.Bw. Njwayo amesema, kabla ya kuuawa kwa
Mwenyekiti huyo, pia wauaji hao walianza kumjeruhi kwa kumpiga risasi ya
tumboni mtoto wa marehemu aliyetajwa kwa jina la Nurdin Iddy
Kirungi.Mganga wa zamu katika kituo cha afya Ikwiriri, Dk. Rashid Omar,
amesema, walimpokea Nurdin akiwa na jeraha kubwa tumboni mwake ambalo
halikutokeza upande wa pili, majeruhi huyo walimpatia rufaa kwenda
Hospital ya Mchukwi kutokana na kuwa anavuja damu nyingi sana.
SHARE









No comments:
Post a Comment