Rasi wa Urusi Vladmir Putin na Rais mteule wa Marekani Donald Trump
Ikulu ya
Urusi imesema kwamba rais Vladimir Putin amezungumza kwa njia ya simu na
rais mteule wa Marekani Donald Trump, pamoja na mambo mengine
amempongeza kwa ushindi aliopata,Putin amesema kwamba anaahidi kufanya
kazi pamoja na rais huyo wa Marekani Donald huku akitilia mkazo suala la
uhusiano wa nchi hizo mbili.
Wakati wa
harakati zake za kampeni, Trump aliendelea kurudia rudia kumpongeza
rais huyo wa Urusi, akimuelezea kama mtu mwenye upeo mkubwa
ukimlinganisha na rais anayeondoka madarakani Barack Obama.
Wakati huo huo.
RAIS
Barack Obama amewahakikishia washirika wa Marekani kwamba Donald Trump
ataendeleza heshima na ushirikiano wa kimataifa baina ya nchi yake nao
wakati yeye atakapokabidhi urais mwezi Januari,Obama ameyasema hayo
wakati alipokuwa na mkutano mkubwa na waandishi habari .Rais Obama
amesema kwamba Donald Trump ameonesha nia ya kutaka kudumisha uhusiano
baina ya Marekani na shirika la nuklia duniani NATO.
Obama
amesema kwamba Marekani lazima iendelee kuwa nguzo ya nguvu na nguzo ya
matumaini kwa watu duniani kote.Na kuongeza kusema kwamba uhusiano baina
ya nchi na nchi unakwenda mbali zaidi ya nafasi ya urais na
wanadiplomasia,majeshi na kwamba wakuu wenye hekima na busara
wataendelea kuonesha ushirikiano na wenzao wanaoshughulikia masuala ya
kigeni.
Obama alikuwa akizungumza kuelekea mwishoni mwa safari zake za mataifa ya kigeni akiwa mwishoni mwa madaraka yake ya urais. BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment