Dk Elias Mwandwani akimpima kisukari mmoja wa wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Mkurugenzi
wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru akiwa
amevaa beji ikiwa ni ishara ya kuwamasisha wafanyakazi wa hospitali hiyo
kupima kisukari.
Juma Selemani akipima uzito Leo kabla ya kupima kisukari katika Hospitali hiyo.
Dk Faraja Chiwanga wa Muhimbili akimpima kisukari Juma Selemani katika hospitali hiyo.
Na Neema Mwangomo
Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH) jana imeadhimisha siku ya kisukari duniani kwa
kuwapima kisukari wafanyakazi wa hospitali hiyo.
Jana wafanyakazi wa hospitali hiyo walikuwa wakipimwa kisukari na uzito pamoja na kupatiwa ushauri jinsi ya kupunguza uzito kwa wale waliobainika kuwa na uzito mkubwa.
Wafaanyakazi waliojitokeza jana ni madaktari, wafanyakazi kurugenzi za utawala, wauguzi na wanafanyakazi mbalimbali wa hospitali hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa hospitali hiyo Profesa Lawurence Museru alikuwa mstari wa
mbele katika kuwashawishi wafanyakazi kupima kisukari.
Naye
Mkuu wa Kitengo cha Kisukari, Dk Mohamed J. Mohamed amesema Muhimbili
imeona kuna umuhimu wa kupima kisukari kwa wafanyakazi wake kutokana na
kubanwa na shughuli mbalimbali na hivyo mara nyingi wamekuwa wakikosa
nafasi ya kupata huduma za afya.
“Tumeona
ipo haja ya kutoa huduma hii kwani kuwa mfanyakazi wa Muhimbili
haimaanishi kwamba upo salama kiafya hivyo tunafanya hivi ili wapate
nafasi ya kupia kisukari,” amesema Dk Mohamed. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment