Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha
RAIS John
Magufuli,ameweka bayana sababu za kuivunja bodi ya mamlaka ya mapato
Tanzania( TRA) kuwa ilikuwa ni baada ya kuidhinisha mabilioni ya fedha
kiasi cha sh.bil 26,katika taasisi binafsi tatu za kifedha.
Amesema
fedha hizo zilikuwa zimetolewa katika mamlaka hiyo kwa ajili ya matumizi
ya TRA na bodi ikapitisha ndio sababu ya kuivunja ambapo fedha hizo
ameshazichukua na zipo kwenye mikono salama.
Dk.Magufuli
aliyasema hayo katika mahafali ya 31,ya chuo kikuu huria
Tanzania(OUT)yaliyofanyika makao makuu ya chuo hicho Bungo wilayani
Kibaha .
Alielezea
kuwa pamekuwa na kamchezo hako ,kwa baadhi ya viongozi wa aina hiyo
ambapo wanachukua fedha za miradi mbalimbali na kuziweka katika mabenki
binafsi kwa mazungumzo baina ya mkuu wa taasisi na taasisi husika.
Aidha
alisema TEA ambayo imeanzishwa kwa ajili ya makusudi maalum na
kuchangiwa fedha kwa ajili ya kujengea madarasa na kusaidia masuala ya
sekta ya elimu zaidi ya sh.bil 30 lakini fedha hizo wameweka kwenye
Fixed Account ili kupata faida.
“Waziri
wa elimu na mafunzo ya ufundi ,upo message sent,mchezo huu upo sana
wanazichukua na kupeleka kwenye Commerce Banks,wanaweka kwenye Fixed
Deposit Accounts kwa makubaliano baina ya mkuu wa taasisi na taasisi za
fedha husika.”
“TEA
imeanzishwa kwa makusudi maalum bil.zaidi ya 30 lakini wamechukua fedha
hizo na kupeleka kwenye taasisi za kifedha ,wakati kwenye elimu watu
wanapata shida,sasa wananchi wakati mkiona serikali inachukua hatua ya
kutumbua mtuachie tuu tuendelee kutumbua”alisema Dk.Magufuli.
Dk
Magufuli alisema kumekuwa na mchezo wa wakuu wa taasisi mbalimbali
kuchukua fedha na kuziwekwa kwenye akaunti maalumu ambapo serikali
inakwenda kukopa kwa gharama kubwa.
“Kwa sasa
huu ndo mchezo ambao unachezwa na kuisababishia serikali kukosa fedha
jambo ambalo serikali haiku tayari kuona matumizi mabaya ya fedha zake,”
“Naomba
mtuombee tuendelee kutumbua kwani nchi ilifika mahali pabaya lakini
sasa tumbua hii mapato yameongezeka na kufikia trilioni 1.2 na kufikia
1.8 ambapo uchumi umeimarika,” alisema Dk Magufuli.
Uchumi
umeimarika kwa asilimia 7 unatakiwa ukue kwa asilimi 7.2 hadi robo ya
mwaka huu umekuwa 7.9 na kuwa moja ya nchi ambazo uchumi wake unakua
ambako kati ya nchi tano imekuwa ya pili baada ya Ivory Coast.
Alisema kuwa suala la ubora wa elimu nchini halina mjadala na hakuna njia ya mkato kupata elimu bora.
Hata hivyo alifafanua kwamba lengo ni kulinda ubora wa elimu inayotolewa ili kuwa na wasomi ambao watakuwa watumishi bora.
Dk
Magufuli alisema kuwa kutokana na kutaka kuhakikisha elimu inatolewa kwa
ubora ambapo hata wale wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
walipohakikiwa walikutwa wenye sifa za kuwa pale ni wanafunzi 322 kati
ya 7,500.
“Tungependa
kila mtu asome kwa sifa aliyonayo na si vinginevyo tungependa sifa ya
elimu yetu iwe kuwa juu na ni bora kuwa na wanafunzi wachache kuliko
kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wasio na sifa,” alisema Dk Magufuli.
Alisema
kuwa serikali ilipoamua kufanya elimu bure kwa shule za msingi na
sekondari kulijitokeza changamoto nyingi ambapo wanafunzi wa shule za
msingi
idadi iliongezeka kwa asilimia 84 kwa shule za msingi na sekondari kidato cha kwanza iliongezeka kwa asilimia 26.
idadi iliongezeka kwa asilimia 84 kwa shule za msingi na sekondari kidato cha kwanza iliongezeka kwa asilimia 26.
“Madawati
tumepambana na sasa imefikia asilimia 98 huku mikoa michache inamalizia
zoezi hilo pia kuliongezeka wanafunzi hewa 65,000 kwa shule za msingi
na sekondari ambao walikuwa wakilipwa malipo hewa kwa kuongezwa majina
ya uongo,” alisema Dk Magufuli.
“Changamoto
zilizidi kuongezeka kwani bajeti ya mikopo iliongezeka kutoka bil. 340
na kufikia bilioni 473 kutokana na ongezeko la wanachuo 98,000 hadi
kufikia 124,389 ambapo wanafunzi waliokuwa wanapewa mikopo hewa kwenye
vyuo hadi sasa imefikia kiasi cha shilingi bilioni 3.5,” alisema Dk
Magufuli.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment