Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Methew Mtigumwe akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wa hadhara Kijijini Doroto
Baadhi
ya wananchi wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi
Methew Mtigumwe katika ziara yake katika Halmashauri ya Itigi
Mkuu wa
Wilaya ya Manyoni Mhe Godfrey Mwambe akiongea na wananchi katika ziara
ya mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Methew J. Mtigumwe
Na Mathias Canal
Mkuu wa
mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Mathew John Mtigumwe jana ameanza ziara ya
kikazi kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika Mkoa
wa Singida.
Rc
Mtigumwe ameanza ziara yake hiyo katika Halmashauri ya Itigi, iliyopo
katika Wilaya ya Manyoni ambapo atatembelea kata zote za halmashauri
hiyo.
Pamoja na
kutambua kero za wananchi na mambo mengine pia Mkuu huyo wa Mkoa wa
Singida anatumia mikutano hiyo maalumu kwa ajili ya kufahamiana na
wanachi ikiwa ni pamoja kusikiliza kero zao ambazo zimewasua kwa miaka
mingi bila kupatiwa ufumbuzi.
Mtigumwe
akiwa katika Kijiji cha Doroto amehimiza zaidi wananchi kuandaa vyema
mashaba yao na kuzingatia kilimo chenye kustahimili ukame kwani kuna
mabadiliko makubwa ya tabia nchi jambo ambalo limepelekea kuchelewa
kuanza kwa mvua.
Mhe
Mtigumwe amewaagiza maafisa kilimo wa Kata na Wilaya zote za Mkoa wa
Singida kutokaa ofisini kipindi hiki cha msimu wa kilimo badala yake
kwenda mashambani kuwasaidia wananchi mbinu bora za kilimo sambamba na
kuwasaidia namna bora ua kuandaa mashamba.
Sambamba
na hayo pia amewasisitiza wananchi kuzingatia maelekezo watakayopatiwa
na Maafisa kilimo ili kuwa na uhakika wa kuvuna mazao mengi zaidi kwa
kilimo chenye tija.
Katika
ziara yake Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew Mtigumwe ameambatana
na Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Singida.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment