Waziri wa
Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akiangalia aina ya bomba
lililotumika kwenye mradi wa Ruvu Chini na Mkurugenzi wa Kiwanda cha
Tanzania Steel Pipes Limited, Nicolas Loh (kulia) pamoja na Meneja
Biashara, Ryan Koh.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akiwa kwenye karakana ya kiwanda hicho.
Mafundi wakiwa kazini katika karakana ya Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited.
Waziri wa
Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akimsikiliza Mkurugenzi wa
Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited, Nicolas Loh na kujionea moja
ya mabomba yanayotengenezwa na kiwanda hicho.
Waziri wa
Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge mwishoni mwa wiki alitembelea
Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited (TSP) kilichopo Shekilango, Dar
es Salaam.
Kiwanda
hicho kinachotengeneza mabomba ya maji, ambayo pia yanatumika katika
utekelezaji wa miradi ya maji nchini, ukiwemo mradi ya maji ya Ruvu
Chini, KASHWASA na Ruvuma.
“Nimeridhishwa
na uwekezaji wa kiwanda hiki cha mabomba, ambacho kina uwezo wa
kuzalisha mabomba yenye ubora wa kutekeleza miradi yetu ya maji nchini”.
“Hii ni
hatua kubwa kwa nchi yetu ikizingatiwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano
imedhamiria kuinua uchumi wa viwanda nchini, hivyo maendeleo ya kiwanda
hiki ni hatua nzuri ya kufikia lengo hilo”, alisema Waziri Lwenge.
Inj.
Lwenge alisema uwezo ilionao kiwanda hiki ni chachu ya maendeleo kwa
Sekta ya Maji na Umwagiliaji kwani kwa muda mrefu Serikali imekuwa
ikununua mabomba kutoka nje ya nchi, na hata yanayotengenezwa hapa mengi
ni ya plastiki ambayo hayadumu muda mrefu ukilinganisha na ya chuma.
Naye
Mkurugenzi wa kiwanda cha Kiwanda cha Tanzania Steel Pipes Limited (TSP)
alisema nia yao kubwa ni kutengeneza bidhaa nzuri zenye ubora wa
kimataifa na kushindana katika soko la kimataifa, na kuiomba Serikali
itumie bidhaa za wawekezaji wa ndani zenye ubora wa hali ya juu.
Alisisitiza
bidhaa zao zinatengenezwa hapa nchini tangu hatua ya awali na wala si
kuagizwa kutoka nje, zina uwezo wa kudumu mpaka miaka 50, zinatumika nje
ya nchi ikiwemo Rwanda, ambapo zinatumika kwenye miradi mikubwa ya
maji.
Dhumuni la ziara hiyo lilikuwa ni kujionea uwezo wa kiwanda hicho kwa upande wa uzalishaji na ubora wa bidhaa zao.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment