Waziri mkuu wa DRC aliyejiuzulu nafasi yake, Augustin Matata Ponyo
Waziri
mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, Matata Ponyo, ametangaza
kujiuzulu nafasi yake, ili kupisha uteuzi wa waziri mkuu mpya ambaye
atatoka kwa vyama vya upinzani vilivyoshiriki mazungumzo ya kitaifa.
Akizungumza
jijini Kinshasa, waziri mkuu Matata Ponyo amesema "nimewasilisha barua
yangu ya kujiuzulu kwa rais pamoja na baraza langu lote la mawaziri, ili
kutimiza matakwa ya makubaliano ya kitaifa yaliyoafikiwa hivi
karibuni," alisema Matata baada ya kukutana na rais Josephu Kabila.
Kujiuzulu
kwake ambako kunaenda sambamba na makubaliano ya kumaliza mzozo wa
kisiasa nchini humo, kumefanyika wakati ambapo makubaliano hayo
yanapingwa vikali na muungano wa upinzani unaoongozwa na Etienne
Tshisekedi wa Mulumba.
Fukuto la
joto la kisiasa liliongezeka zaidi mwezi uliopita baada ya kuahirishwa
kwa uchaguzi mkuu ambao kwa mujibu wa katiba ulikuwa umepangwa kufanyika
mwishoni mwa mwaka huu lakini sasa umeahirishwa hadi mwezi April 2018.
Kiongozi wa upinzani nchini DRC, Vital Kamerhe ambaye ametengwa na muungano wa upinzani
Upinzani
unamtuhumu rais Kabila, ambaye amekuwa madarakani toka mwaka 2001 kwa
kuichezea katiba ya nchi hiyo ili asalie madarakani wakati muhula wake
wa pili na wa mwisho utakapotamatika.
Uamuzi wa
kuahirisha uchaguzi, ulichukuliwa mwezi Octoba mwaka huu na Serikali,
uamuzi ambao ukasababisha kuundwa kwa timu maalumu itakayoshiriki
mazungumzo ya kitaifa ili kupata suluhu, makubaliano ambayo hata hivyo
yamekashifiwa na baadhi ya viongozi wa upinzani.
Rais Josephu Kabila anatarajiwa kulihutubia taifa Jumanne ya wiki hii, Novemba 15, katika hotuba atakayoitoa bungeni.
Etienne Tshisekedi, kiongozi wa muungano wa upinzani unaopinga makubaliano ya kitaifa, hapa ni Novemba 1, 2016
Ujumbe wa
baraza la usalama la umoja wa Mataifa ulioko nchini DRC, umetoa wito wa
mabadilishano ya amani ya utawala nchini humo, kufuatia hofu ya kuzuka
vurugu.
Kiongozi
wa chama cha UNC, Vitaly Kamerhe ambaye chama chake kilishiriki kwenye
mazungumzo hayo ya kitaifa, anatajwa tajwa kuchukua mikoba ya waziri
mkuu Matata Ponyo.
Katika
mawaziri wakuu wote ambao nchi ya DRC imewapata kwa kipindi cha miaka 56
iliyopita, Matata Ponyo ndiye waziri mkuu pekee ambaye amedumu kwa
kipindi kirefu katika wadhifa huo.RFI
SHARE
No comments:
Post a Comment