WASANI
202 wa mikoa ya kanda ya ziwa wajiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF
kupitia mfumo wa uchangiaji wa hiyari wa Wote Scheme jijini Mwanza
wakati wa warsha fupi ya kuwajengea uwezo wa sanii iliyofanyika katika
ofisi ya mkuu wa Mkoa jijini Mwanza.
Akizungumza
wakati wa kuwakabidhi kadi za uanachama wasanii hao Meneja wa PPF Kanda
ya ziwa, Meshack Bandawe amesema wasanii mbali mbali wamejiunga katika
mfumo ‘Wote Scheme’moja kwa moja katika Mfuko huo ambapo watapata
mafao yanayotolewa na PPF
moja kwa moja katika mfumo wa Wote Scheme ambapo mtaweza kupata huduma ya matibabu baada ya kuchangia miezi 3,
faida ni kupata mikopo ya biashara, pamoja na mafao ya uzeeni.
Amewaasa
wananchi wote wa mikoa ya kanda ya ziwa ambao hawapo katika sekta rasmi
kama madereva wa Tax, wajasiliamali, wakulima, wavuvi, wafanyabiashara
na madereva wa bodaboda wajiunge na mfuko wa PPF ili waweze kunufaika na
mafao mbali mbali.
Wasanii
hao ni kutoka Mwanza, Mara, Shinyanga, Simiyu, Tabora na Geita, pamoja
na kupata elimu kutoka PPF vilevile washiriki walipata fursa ya
kujengewa uwezo wa kuhariri kutengeneza Miswada ya filamu pamoja na
umuhimu wa kujiunga na mifuko ya uchangiaji wa hiari kwa ajili ya
manufaa yao wenyewe pamoja na familia zao.
Kwa
upande wa wasanii wamefurahia sana mfumo wa Wote scheme kwani umekuja
wakati sahihi ambapo Mfumo huu wa PPF utawasadia kwa kuwezesha kupata
mikopo ya maendeleo na Bima ya afya, hivyo kuwafanya kuendelea na maisha
yao.
Meneja
wa PPF Kanda ya ziwa, Meshack Bandawe akimkabidhi mfano wa kadi ya
uanachama wa Mfuko wa PPF, Msanii wa Filamu jijini Mwanza, Mwanaharusi
Hela ambapo zaidi ya wasanii 202 walipojiunga na na mfuko wa PPF
mwishoni mwa wiki katika warsha ya kuwajengea uwezo wasanii wa mikoa ya
kanda ya ziwa jijini Mwanza leo.
Meneja
wa PPF Kanda ya ziwa, Meshack Bandawe akizungumza na baadhi ya wasanii
wa mikoa ya kanda ya ziwa mara baada ya kuwakabidhi kadi za uanachama mara baada ya kujiunga na mfuko huo mwishoni mwa wiki.
Meneja
wa PPF Kanda ya ziwa, Meshack Bandawe pamoja na baadhi ya wafanyakazi
wa PPF akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasaniiwaliojiunga na
PPF kupitia mfumo wa Wote Scheme.
Msanii
wa filamu Mwanaharusi Hela akizungumza jinsi alivyofurahishwa na
mfumo wa wote scheme kupitia PPF ambapo utamnufaisha kwa kupata huduma
ya afya na mkopo wa maendeleo.
Msanii
na mpiga picha wa filamu akichangia maada wakati wa warsha ya siku tatu
ya kuwajengea uwezo wasanii wa Mikoa ya kanda ya ziwa iliyofanyika
jijini Mwanza.
Afisa
uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF jijini Mwanza, Mohamed Nyengi
mwenye tisheti nyeupe akitoa maelekezo jinsi ya kujaza fomu ya kujiunga
na mfuko wa uchangiaji wa hiari wa PPF (Wote Scheme) ambapo PPF iliweza
kutoa semina kwa washiriki umuhimu wa kuchangia na Mfuko wa Pensheni wa
PPF.
Afisa
uendeshaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF jijini Mwanza, Mohamed Nyengi
kulia akitoa maelekezo kwa wasanii wa mikoa ya kanda ya ziwa jijini
Mwanza.
Msanii
akijaza fumu ya kujiunga na uanachama wa mfuko wa PPF jijini Mwanza
mara baada ya kuhudhuria warsha ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wasanii
hao jijini Mwanza.
SHARE
No comments:
Post a Comment