Mkutano
wa Umoja wa Ulaya ambapo viongozi 27 wanatarajiwa kuafikia makubaliano
kuhusu mazungumzo ya kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja huo ulizua
hali ya kutoelewana pale wabunge walipotaka jukumu kubwa zaidi
Ijapokuwa
bunge la Umoja wa Ulaya litabidi kuidhinisha hatua yoyote ya kujiondoa
kwa Uingereza katika muungano huo baada ya mazungumzo hayo, mataifa ya
Umoja huo yanapanga kumteuwa Michel Barnier kuwa mpatanishi mkuu na
kuliachia bunge hilo kutekeleza jukumu dogo.
Katika
pendekezo la bunge hilo lililoonekana na shirika la habari la Associated
Press, wabunge hao wanataka kuhudhuria vikao vyote vya mazungumzo hayo.
Afisa mkuu wa bunge hilo katika mazungumzo hayo Guy Verhofstadt,
ametishia kuanzisha mazungumzo sambamba na Uingereza.
Verhofstadt
aliongeza kuwa, iwapo baraza hilo halitalitaka bunge hilo katika chumba
hicho cha mazungumzo basi litaanzisha mashauriano moja kwa moja na
Uingereza.
May atoa wito wa mpangilio katika kujiondoa kwa Uingereza
Wakati
huohuo, waziri mkuu wa Uingereza Theresa May amewahimiza wenzake katika
Umoja wa Ulaya kuhakikisha kuwa hatua ya Uingereza ya kujitoa katika
Umoja huo inatekelezwa kwa njia shwari huku wanapojiandaa kujadilia
suala hilo hii leo katika dhifa ya jioni ambayo hatahudhuria.
Mbali na
suala hilo la kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja huo, Rais wa ufaransa
Francois Hollande alisema kuwa anawataka viongozi katika mkutano huo
kutoa wito wa kusitishwa kwa mashambulizi mjini Aleppo kuwawezesha raia
na majeruhi kuhamishwa kutoka eneo hilo.
Akitaja
mpango wa kuhakikisha usalama katika mji huo nchini Syria, aliwaambia
wanahabari kuwa kwa haya yote kuwezekana , pendekezo la kusitishwa kwa
mashambulizi lazima litekelezwe na huu ndio wito unaopaswa kutolewa na
Umoja wa Ulaya .
Rais wa
Umoja huo wa Ulaya Donald Tusk anatarajiwa kukutana na meya wa Aleppo
Brita Hagi Hassan aliye mjini Brussels kushinikiza Umoja huo kuunga
mkono kufunguliwa kwa njia ya mashirika ya misaada ya kibinadamu
kuwahamisha raia kutoka eneo hilo.
Viongozi
hao watatoa taarifa kwamba Umoja wa Ulaya unashtumu vikali mshambulizi
yanayotekelezwa na serikali ya Syria na washirika wao Urusi na kusema
kuwa Umoja huo unakadiria njia zote zilizoko, kulingana na rasimu
iliyoonekana na shirika la habari la AFP:
Mkutano
huo pia unalenga kuangazia masuala mengine kama vile kukabiliana na
uhamiaji kutoka Afrika na kuimarisha ulinzi dhidi ya Urusi huku Donald
Trump akijitayarisha kuchukuwa uongozi wa Marekani, agenda inayowatia
hofu waingereza wengi kwamba huenda ikatatiza hatua ya Marekani ya
kujitolea kuwalinda dhidi ya Urusi.DW
SHARE
No comments:
Post a Comment