WINGA wa
kushoto wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Farid
Mussa, ameweka wazi kuwa mabingwa hao hawajambania kwenda nchini
Hispania kucheza soka la kulipwa kama ilivyoripotiwa na vyombo
mbalimbali vya habari.
Kwa
kuudhihirishia umma, Mussa leo amejitokeza hadharani na kupinga madai
hayo akidai kuwa muda wowote kuanzia sasa atakwenda nchini humo kujiunga
na Club Deportivo Tenerife inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza baada ya
kupata ‘Visa’ maalumu ya kuingia nchini akiwa kama mfanyakazi.
“Kwanza
napenda kumshukuru Mungu baada ya kupata visa, haikuwa kazi rahisi
namshukuru Meneja Mkuu Abdul (Mohamed) kapigania hadi suala hili
limekamilika, cha kwanza nilikuwa ninawaomba Watanzania wajue kuwa Azam
haikuwa inanibania ni masuala tu ya visa yalikuwa yakisumbua ubalozini.
“Mara
baada ya kupata visa ya kufanya kazi muda wowote ninaweza kuondoka
kuanzia Januari,” alisema Farid wakati akizungumza mbele ya waandishi wa
habari leo wakati wa zoezi la kutambulishwa wachezaji wapya
waliosajiliwa na timu hiyo.
Taarifa
hizo zilianza kutolewa kwenye vyombo vya habari, kufuatia suala la Farid
kwenda Hispania kuwa kimya lakini ukweli wa mambo ni kuwa visa hiyo
ndio iliyokuwa ikikwamisha dili hilo.
Naye
Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd, akitolea ufafanuzi suala hilo
alisema kuwa lengo la uongozi huo lilikuwa ni kinda huyo kuondoka mapema
kuelekea nchini humo, lakini suala kubwa lilikwamisha ni visa hiyo ya
kufanya kazi nchini Hispania.
“Uongozi
wa Azam FC ulikuwa sambamba na Tenerife kuhakikisha Farid anaondoka,
lakini tunashukuru suala hilo limekamilika kwa asilimia 98, lakini ni
kwamba Farid muda wowote kuanzia sasa Mungu akijaalia ndani ya wiki
mbili zijazo au wiki moja anaweza kuondoka kutoka Tanzania kuelekea
Hispania,” alisema.
Azam FC
inaamini ya kuwa kuondoka kwa nyota huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania
‘Taifa Stars’ kutafungua milango kwa wachezaji wengine ndani ya timu
hiyo na Taifa kwa ujumla kuweza kupata nafasi ya kucheza soka la kulipwa
barani Ulaya.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment