Meya wa
jiji la Mbeya David Mwashilindi akisaini Mkataba kwa ajili ya uboreshaji
wa Miundombinu ya barabara katika jiji la Mbeya.
Na JamiiMojaBlog
HALMASHAURI
ya Jiji la Mbeya, leo imeingia mkataba na makandarasi mbalimbali wa
ujenzi wa miundombinu ya barabara pamoja na madaraja katika Kata 14.
Mkataba
huo, umesainiwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, David Mwashilindi
huku ukishuhudiwa na baadhi ya madiwani wa Kata husika pamoja na
mwanasheria wa halmashauri hiyo Davis Mbembela.
Awali
akizungumzia tukio hilo kabla ya kusaini, Meya Mwashilindi amesema,
mkatba huo, unalenga kuboresha miundombinu katika baadhi ya kata katika
halmashauri hiyo ambapo kazi hiyo inataraji kuanza mapema mwezi huu.
Aidha,
amesema kuwa mkataba huo unagharimu kiasi cha shilingi milioni 300 na
kwamba kazi kubwa itakayofanyika ni uboreshaji wa barabara na
matengenezo ya madaraja katika kata 14 kati ya 36 zilizomo ndani ya Jiji
la Mbeya.
“Kampuni zilizoingia mkataba leo ni tano na zote ni makandarasi wa ndani na kubwa zaidi ni wazawa,”amesema.
Pia,
Mwashilindi amewataka makandarasi waliochukua kazi hizo kuhakikisha
wanafanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa na kwa muda muafaka huku
akiwatoa hofu juu ya fedha, kwani bajeti ya matengenezo hayo tayari
imeidhinishwa..
Hata
hivyo, katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa asilimia 100,
Mwashilindi amewataka watendaji pamoja na madiwani kuhakikisha
wanatembelea na kukagua miradi hiyo, wakati ikiendelea kufanyika na
kuachana na tabia ya kusubili mradi ukamilike na kukabidhiwa na ndipo
kuanza kubaini kasoro.
“Serikali
imekuwa ikitumia fedha nyingi na asilimia kubwa inatokana na kodi za
wananchi hivyo ninawaombeni madiwani na watumishi hasa wa idara husika
kuhakikisha mnatembelea na kuukagua mradi huu wakati wote wa mchakato,
sitapenda kusikia changamoto mara baada ya mradi kukamilika,”amesema.
Baadhi ya
Wakandarasi wa makampuni mbalimbali ya jiji la Mbeya wakisaini mikataba
kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara katka baadhi ya kata
jijini Mbeya
Baadhi ya
Wakandarasi wa makampuni mbalimbali ya jiji la Mbeya wakisaini mikataba
kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara katka baadhi ya kata
jijini Mbeya hafla ambayo imehudhuriwa pia na baadhi ya madiwani na
watendaji wa halmashauri ya jiji katika ofisi ya Meya .(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment